3293; Njia ya kuepuka kifo.

Rafiki yangu mpendwa,
Kila ambacho kimezaliwa au kuanzishwa, safari yake huwa inaishia kwenye kifo.
Hiyo siyo tu kwa viumbe hai, bali kwa vitu vyote.

Mwenendo wa kila kitu huwa una mwendo ambao uko dhahiri kabisa. Huo ndiyo mzunguko ambao mtu unapaswa kuutumia vizuri ili kuepuka kifo.

Mzunguko wa maisha ya kitu chochote kile uko kama ifuatavyo;
1. Ukuaji wa kasi.
2. Kuridhika.
3. Kudumaa.
4 Kushuka.
5. Anguko.

Kila kitu huwa kinapitia mzunguko huo, tangu kuanza mpaka kifo.

Kuna vitu ambavyo hutaki vife kizembe, kimoja wapo kikiwa biashara unayojenga.
Unataka iwe ni biashara itakayodumu kwa vizazi vingi vijavyo.

Ili hilo lifanikiwe, kifo cha biashara kinapaswa kuwa kitu ambacho kinaepukwa sana.

Ili kuweza kuepuka kifo cha biashara, unapaswa kurudi kwenye mzunguko wa maisha ya biashara na kuchagua eneo la kuwekea kazi ili kuzuia mengine yasiendelee.

Eneo zuri la kuwekea kazi ili kuepuka kifo ni Ukuaji wa kasi.
Kupitia kuwa na ukuaji wa kasi na ambao ni endelevu, biashara inaendelea kuwa hai na kuepuka kifo.

Kikubwa sana ni kuepuka hatua inayofuata ambayo ni ya kuridhika.
Hapo ndipo anguko huwa linaanzia.

Kinachohitajika ni kupambania ukuaji wa kasi mara zote na kuepuka kuridhika au mazoea.

Ni jambo linalohitaji kasi kubwa kwenye kulifanyia kazi, lakini matokeo yake ni mazuri.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe