3295; Ufuatiliaji wa karibu.
Rafiki yangu mpendwa,
Kitu kimoja ambacho nimejifunza kwenye kupata chochote unachotaka ni ufuatiliaji wa karibu unalipa sana.
Mara nyingi sana huwa hupati kile unachotaka kwa mara ya kwanza unapokuwa unakitaka.
Huwa kuna kizuizi fulani ambacho kinakuwepo.
Baada ya kizuizi hicho, kupata au kutokupata unachotaka, huwa kunategemea sana ufuatiliaji wako.
Unapokuwa unataka chochote kutoka kwa watu, huwa wanakupa ahadi za wakati wa mbele.
Kutimia kwa ahadi hizo inategemea sana ufuatiliaji wako.
Ili upate chochote unachotaka, lazima uwe na ufuatiliaji wa karibu, kwa mwendelezo na bila ya ukomo.
Unapokuwa king’ang’anizi wa ufuatiliaji, unapata kile unachotaka.
Na kama unataka matokeo ya haraka au mambo yaende haraka, basi fuatilia mara kwa mara, kila baada ya muda mfupi.
Kufupisha muda wako wa kufuatilia kunapeleka ujumbe kwamba kitu ni muhimu na hivyo upande wa pili kuchukua hatua haraka zaidi.
Watu wengi ambao hawana ujasiri wa kukukatalia kwenye kile unachotaka, huwa wanakupa ahadi hewa, wakijua kwa uvivu na uzembe wako hutakumbuka kufuatilia.
Wengine wanaamua wakuchoshe kwa kila wakati kukupa ahadi mpya.
Unapokutana na watu wa aina hii, ambao wanashindwa kukukatalia ila wanakupa ahadi nyingi hewa, kwanza furahia, maana hapo una uhakika wa kupata unachotaka.
Halafu sasa, fuatilia kadiri ya ahadi zao. Wamekuahidi, fuatilia kama walivyoahidi. Wakikupa ahadi nyingine, fuatilia hivyo pia.
Nenda na hizo ahadi bila kuchoka wala kuacha.
Mpaka watalainika wenyewe na kukupa unachotaka.
Fuatilia kama mtu aliyeingiwa na wendawazimu.
Wafanye watu waone kitu ni muhimu sana kutokana na ufuatiliaji wako wa msisitizo na usiokoma.
Ahadi yoyote unayopewa, wewe fuatilia bila kuchoka.
Mara nyingi sana, kupata unachotaka, unapaswa kuuchosha upande wa pili.
Unapaswa kulainisha ugumu ambao unawekewa.
Na hayo yote ni kupitia ufuatiliaji endelevu na usiokuwa na ukomo.
Mengi sana ambayo umeyakosa kwenye maisha yako ni kwa kushindwa kufuatilia.
Ahadi nyingi zimepotea kwa kushindwa kufuatilia.
Hapana nyingi ulizopewa na ukazikubali ni ulishindwa tu kufuatilia kwa karibu ili kuzigeuza kuwa ndiyo.
Ufuatiliaji una nguvu kubwa sana unapofanyika bila ya ukomo.
Fuatilia kama mbwa mwenye njaa aliyeuona mfupa, ng’ang’ana mpaka upate kile unachotaka.
Usikubali kukwamishwa na chochote kile.
Fuatilia, fuatilia na fuatilia tena.
Kama bado hujapata unachotaka, hupaswi kukatishwa tamaa na chochote.
Wewe fuatilia, utapata mengi mazuri kuliko usipofuatilia.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ufuatiliaji wa karibu mara zote utanipa ninachotaka.
LikeLike
Uhakika
LikeLike
Ni kufiatilia.Nitaendelea kufuatilia mpaka nipate ninachokipata kutoka kwa wateja.
LikeLike
Kufuatilia mara nyingi ili kuondoa ugumu uliowekewa na
Hayo yote ni kupitia ufutiliaji endelevu.
🙏🙏🙏
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Ili nipate chochote ninachotaka, lazima niwe na ufuatiliaji wa karibu, kwa mwendelezo na bila ya ukomo,Ninapo kuwa King’a ng’anizi wa ufuatiliaji, nitapata kile ninachotaka.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ufuatiliaji wa karibu bila kuchoka Ndiyo njia ya uhakika ya kupata ninachokitaka.
Nimegundua hii siyo kwa wateja tuu hata kwa wafanyakazi wetu, mara nyingi usipofuatilia waliyokuahidi au mliyokubaliana yafanyike Huwa hayafanyiki.
Siri ya kukamilisha chochote ni kufuatilia Hadi kikamilike
LikeLike
Kil ahadi inatakiwa kufuatiliwa kwa uhakika sana.
LikeLike
Kama bado hujapata unachotaka, hupaswi kukatishwa tamaa na chochote.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Ufuatiliaji una nguvu sana unapofuatilia bila ukomo
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kufuatilia kweli ni kitu bora sana
LikeLike
Tufuatilie.
LikeLike