3296; Hakuna kingine muhimu.
Rafiki yangu mpendwa,
Sababu namba moja ya watu wengi kushindwa kupata matokeo makubwa waliyokuwa wanayataka ni kutawanya nguvu zao kwenye mambo mengi.
Wanakuwa wanapambania vitu vingi kwa wakati mmoja, kitu ambacho kinapunguza ufanisi wao.
Kwa sababu hata kama watapata matokeo, yanakuwa ni ya kawaida sana.
Matokeo makubwa sana huwa yanapatikana pale mtu anapoweka rasilimali zake zote kwenye kitu kimoja.
Anachagua kitu kimoja tu ambacho ndiyo kinakuwa muhimu zaidi kwake.
Hapo anakuwa hakuna kingine muhimu kwake isipokuwa hicho alichochagua.
Baada ya kuchagua kitu kimoja ambacho ndiyo pekee muhimu, anapaswa kuyataka sana matokeo anayokuwa anayategemea.
Yaani kitu pekee anachokuwa anakiona kwenye hicho anachofanya ni yale matokeo anayokuwa anategemea kuyapata.
Kila wanapoangalia, wanachoona ni yale matokeo makubwa wanayokuwa wanayataka.
Hivyo ufanyaji wao wote unakuwa umesukumwa na matokeo hayo.
Hakuna namna anapokea kingine chochote chini ya kile anachotaka kupata.
Kwa kukataa kupokea vitu vya chini, moja kwa moja anakuwa amejipandisha juu na kupokea vilivyo juu kweli.
Jambo moja la kushangaza kuhusu dunia ni pale unapokataa kupokea chochote chini ya unachotaka, unapata unachotaka.
Chagua kile hasa unachotaka, puuza vingine vyote. Weka jugudi kubwa. Kataa matokeo yoyote ya chini ya unayoyategemea.
Ukidhamiria hayo kweli, utaweza kufanya makubwa sana kwenye maisha yako.
Ukihangaika na mengi, hupati chochote kikubwa. Unatawanya sana nguvu zako bila ya mafanikio makubwa.
Ukihangaika na kimoja, unajiongezea uhakika wa kukipata.
Ni juu yako kuchagua njia ipi uende nayo, kwa sababu hakuna mwingine anayeweza kukufanyia maamuzi hayo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Hakuna wa kunifanyia maamuzi,nachagua kutegemea matokeo makubwa na sipokei chochote chini ya kiwango.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante Kocha,
Ni muhimu kuwa na vyanzo Vingi vya kipato. Lakini ni muhimu zaidi kuwa na msimamo kwenye kuweka nguvu na rasilimali zako zote kujenga chanzo kimoja hadi kijiendeshe bila uwepo wako, ndiyo uende kujenga kingine.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Lengo langu kuu ni kuwa mimi halisi kwangu na kupata kile ambacho nina msukumo mkubwa wa ndani yangu kukipata, mengine yote hayana umuhimu mkubwa kwangu; nitaamin zaidi maoni yangu kuliko maoni ya wengine, kwa sababu hayo ndiyo yaliyobeba ukweli kuhusu mimi.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ntaweka rasilimali zote kwenye kitu kimoja na kuuza mengine yote
🙏🙏🙏
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Ni juu yako kuchagua njia ipi uende nayo, kwa sababu hakuna mwingine anayeweza kukufanyia maamuzi hayo.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Nakataa kupokea chochote chini ya ninachotaka ili kupata ninachotaka.
LikeLike
Safi
LikeLike
Fanya kitu kimoja na utapata matokeo makubwa
Asante
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ni kweli hili kqangu limeniathiri sana hasa upande wa biashara nimekua natoka kwa biashara natokomea porini hata wiki
Lakini pia hukp naenda kutawanya pesa na hata nguvu zangu muda ndiyo usiseme
Nimejifunza mengi sana baada ya kuwa chini ya kocha Makirita Amani
LikeLike
Vizuri sana, zingatia ili usirudie makosa.
LikeLike
Upo sahihi kabisa
LikeLike
Ndiyo
LikeLike