💯KCM2324074; Kisichoonekana.

Tumejipata, Tunaachilia Breki.

#AlhamisiYaUbunifu

Mwanamafanikio,

Mwaka wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kufanyia kazi kwa ukubwa kitu kimoja mpaka kitupe mafanikio makubwa tunayoyataka.

Tumeachilia breki kwa kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kujipa uhakika wa kufanya makubwa.

0678 977 007 kupata vitabu.



💯 Neno la leo; Kisichoonekana.

Leo ikiwa ni #AlhamisiYaUbunifu tunaona jinsi ambavyo ubunifu ni kuona kile kisichoonekana kwa nje.

Huwa tunaona watu ni wabunifu pale wanapofanya kitu ambacho hatukutegemea kama kingeweza kufanyika.
Kinakuwa ni kitu kipya kabisa na chenye manufaa.

Lakini chanzo cha ubunifu wowote ule ni mtu kuona kitu ambacho hakionekani kwa nje na kwa wengi.
Mtu anakuwa anaona kitu kwa ndani na anachokamilisha ni kukidhihirisha tu.

Chukua mfano wa mtu anayechonga kinyago. Anakuwa na kipande cha mti au jiwe, wakati wengine wanaona ni mti tu au jiwe tu, yeye anaona kitu cha tofauti ndani yake.
Hivyo anachofanya ni kuondoa vitu ambavyo havihusiki ili kubaki na kile anachotaka.
Anaondoa yale ya ziada ili kudhihirisha kile ambacho anaona kwa ndani.

Ili tuweze kuwa wabunifu, tusiishie tu kuangalia kile kinachoonekana, bali tuangalie na vile visivyoonekana.
Tusidhani kitu hakipo au hakiwezekani kwa sababu hatukioni kwa nje.
Badala yake tuanzie ndani yetu na tuone kwenye kitu kile kisichoonekana.
Tukishaona hicho kisichoonekana, kinachofuata ni kukidhihirisha.

Tunadhihirisha kitu kwa kuondoa yale ambayo hayahusiki.
Na hapo tunabaki na kile ambacho tulikuwa tunakiona ambapo kwa wengine unaonekana kuwa ubunifu mkubwa.

Achilia breki zinazokuzuia kufanikiwa kwa kuwa mbunifu, kwa kuona kilicho ndani pale wengine wanapoangalia nje peke yake na utaweza kufanya makubwa.

💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.

Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu hatari kubwa kwenye maisha yako. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2024/01/11/3298

Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku ya kuona visivyoonekana kwa nje ili kuwa na ubunifu na kufanya makubwa.

Kocha.
💯