3299; Uhakika wa kushinda au kushindwa.
Rafiki yangu mpendwa,
Kwenye maisha, kushinda au kushindwa ni vitu ambavyo mtu anachagua mwenyewe.
Hayo huwa siyo matokeo ya nje kama wengi wanavyodhani.
Bali ni maamuzi ya ndani ya mtu mwenyewe.
Mtu anakuwa na uhakika wa kushindwa pale;
1. Anaposema anajaribu kufanya kitu. Kujaribu kufanya kitu ni kukubali kushindwa. Maana majaribio yanapokea kushindwa kama sehemu ya matokeo.
Kuondokana na hilo acha kuwa mtu wa kujaribu na fanya. Mara zote fanya kwa uhakika na utaweza kufanya kwa ushindi.
2. Unapokuwa na machaguo mengi mbadala. Pale unapokuwa na machaguo mengi mbadala ya vitu vya kufanya pale kile unachoanza nacho kinashindwa, ni kukubali kushindwa. Huwezi kupambania kitu hasa kama una machaguo mengi mbadala. Unapokutana na magumu na changamoto, unakimbilia kwenye chaguo jingine na siyo kukomaa na kile unachofanya.
Kuondokana na hilo futa machaguo yote mbadala uliyonayo na komaa na kitu kimoka pekee. Kitu hicho kimoja kipe kila kinachopaswa kutolewa ili kupata matokeo ya uhakika.
3. Unapokataa kulipa gharama halisi ya mafanikio unayotaka. Kila kitu kwenye maisha kina gharama, hakuna chochote kinachopatikana bure. Kadiri mtu anavyotaka mafanikio makubwa, ndivyo pia gharama ya kulipa inavyokuwa kubwa.
Kwenye mafanikio, gharama kubwa ya kulipa ni kutoa kafara. Hapo ni kuachaba na vitu vizuri na unavyopenda lakini ni kikwazo kwako kupata mafanikio makubwa unayoyataka.
Kuondokana na hilo kuwa tayari kulipa kila aina ya gharama unayopaswa kulipa ili kupata unachotaka. Toa kafara ya kila kitu ili upate mafanikio makubwa unayoyataka.
Ni pale unapokitaka kitu hasa, huku ukiwa huna namna nyingine ndiyo unakuwa umejitoa hasa kufikia mafanikio makubwa.
Kingine chochote nje ya hapo ni kukubali kushindwa kwa uhakika.
Wewe ikatae kabisa hiyo njia ya kushindwa ili uweze kupata ushindi wa uhakika kwenye maisha yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante sana kocha kwa makala nzuri nitaepuka kuwa na machaguo mengi
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Napaswa kujitoa kweli kwenye kile ninachokitaka huku nikiondoa machaguo mengi.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Hapa ndipo tunatambua umuhimu wa kukaa kwenye msimamo sahihi ili kuepuka kelele nyingi na machaguo ya kila mara.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Fanya kitu kimoja mpaka kikuletee mafanikio makubwa
Asante
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Sina chaguo lingine, Sina mbadala mwingine,ni biashara yangu hii tuu. Nitajipa Kila kinachohitajika Ili iweze kusimama na kujiendesha yenyewe, nimeamua hasa kufanya na siyo kujaribu. Nina uhakika wa kushinda, hakuna cha kuniuzia!
LikeLike
Safi sana,
Pambana.
LikeLike
Kila kitu kwenye maisha kina gharama kubwa ya kulipa.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ni pale unapokitaka kitu hasa, huku ukiwa huna namna nyingine ndiyo unakuwa umejitoa hasa kufikia mafanikio makubwa.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Hakuna Mbadala Wala kurudi Nyuma. Hakuna kupoa mpk kieleweke. Ufujara na Umasikini ni Dhambi kwangu na hakina Mbadala Kama pumzi.
LikeLike
Tukatae kabisa.
LikeLike