Kila mtu anataka mafanikio makubwa. Lakini ni wachache wanaoyapata mafanikio hayo kwa uhakika. Wengi wanayakosa mafanikio, licha ya kuzijua siri nyingi za mafanikio na hata kuzifanyia kazi.

Kinachowakwamisha wengi wasifanikiwe ni kuhangaika na mambo mengi ambayo wanadhani yanaweza kuwapa mafanikio, ila hilo halitokei. Sababu kubwa ikiwa ni kwamba wanakuwa hawajayafanya mambo hayo kwa ukubwa wa kutosha.

Kuweka juhudi zako kubwa kwenye mambo machache na kuyafanya kwa ukubwa sana kunakuwa na tija kuliko kuzitawanya juhudi hizo kwenye mambo mengi.

0678 977 007 kupata kitabu.

Pale unapokuwa hujapata chochote unachotaka kwenye maisha yako, sababu huwa ni mbili; KUTOKUJUA na KUTOKUFANYA.

Moja ni unakuwa hujui nini unataka au hujui jinsi ya kupata kile unachotaka. Hilo linawakwamisha wengi ambao huwa wanajikuta wakihangaika na mengi yasiyokuwa na tija kwao.

Na mtu anaweza kujua anachotaka na jinsi ya kukipata ila bado asichukue hatua ili kukipata. Hapo mtu anashindwa kufanya kile anachopaswa ili apate anachotaka.

Kwenye hayo mawili ndiyo unaweza kuweka nguvu kubwa na kupata mafanikio makubwa. Mambo hayo ni KUJIFUNZA kwa kina na KUFANYA kwa ukubwa. Yaani unatakiwa kujifunza sana na pia unatakiwa KUFANYA KAZI kwa juhudi kubwa.

Jifunze kuliko watu wengine wote wanaofanya kile unachofanya, kijue kwa kina na kwa undani na hilo litawafanya wengi wakuamini na kutaka kujihusisha na wewe.

Kwa kuwa kujua pekee hakutoshi, unapaswa kufanya pia. Fanya kwa juhudi kubwa kuliko wengine wote, kuwa mchapakazi ambaye hakuna mwingine anayefanya kama wewe. Na hilo litakuweka mbele ya wengine kwenye kupata kile unachotaka.

Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA nimeeleza kwa kina jinsi ya kutumia mambo hayo mawili kuweza kufanya makubwa kwenye maisha yako. Karibu usikilize kipindi hiki hapo chini.

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

0678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 2. KISIMA CHA MAARIFA, 3. CHUO CHA MAUZO na 4. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.