3305; Jiamini, amua.
Rafiki yangu mpendwa,
Kila mtu kwenye maisha anajua nini hasa anachotaka kupata na nini hasa anachopaswa kufanya ili kupata anachotaka.
Hayo yapo wazi kabisa kwa mtu, lakini kwa nje inaweza kuonekana tofauti.
Kwa nje watu wengi wanaonekana kama hawajui nini wanataka na nini wanapaswa kufanya ili kupata matokeo ya tofauti.
Wengi wanakwepa kufanya maamuzi kwa sababu hawataki kuwajibika pale mambo yanapokwenda tofauti.
Hawataki lawama kama mambo yataharibika.
Hivyo wengi wanaishia kutoa mapendekezo ambayo hayawawajibishi sana.
Unapaswa kujiamini wewe mwenyewe na kufanya maamuzi ambayo utayasimamia kwa uhakika na kuwajibika nayo.
Kila dakika ambayo unachelewa kufanya maamuzi, wengine tayari wanachukua hatua kubwa kwenye eneo hilo.
Hao wanaokutangulia wanajijengea nguvu kubwa ya kujihakikishia kupata wanachotaka.
Unapojikuta njia panda na hujui kama uelekee kulia au kushoto, wenzako tayari wameshachukua njia wanayotaka na wanapata manufaa.
Ambao tayari wanachukua hatua siyo kwa sababu wana uwezo mkubwa sana, bali ni kwa sababu wanajiamini wao wenyewe na kufanya naamuzi kisha kuchukua hatua.
Kwenye haya maisha, unapaswa kufanya maamuzi au utafanyiwa maamuzi.
Unapaswa kujituma la sivyo utatumwa.
Na unapaswa kuwa na malengo yako ambayo unayapambania, la sivyo utatumika kupambania malengo ya wengine.
Ukijisikiliza wewe mwenyewe, yote tuliyojifunza hapa tayari yapo ndani yako na unayo majibu sahihi.
Unachohitaji wewe ni kujiamini, kufanya maamuzi na kutekeleza maamuzi hayo kwa uhakika.
Yote hayo yanawezekana kabisa, lakini lazima yaanze na wewe mwenyewe.
Anza kufanyia kazi hilo kwa kuchukua hatua ndogo ndogo kwenye maisha yako ya kila siku.
Hatua unazopaswa kuchukua ni kufanya maamuzi na kuyatekeleza kwenye kila unachotaka.
Kwa kwenda hivyo utaweza kukamilisha makubwa unayotaka kukamilisha kwenye maisha yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kufanya maamuzi na kuyatekeleza.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Asante Kocha,
Ili nifanye makubwa ninachohitaji ni kujiamini, kufanya maamuzi na kuyatekeleza maamuzi hayo kwa uhakika.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Kwenye haya maisha usipojitawala utatawaliwa
Asante sana
LikeLike
Tena utatawaliwa vibaya sana.
LikeLike
Kwenye haya maisha usipojitawala, utatawaliwa
Asante sana
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Wengi wanakwepa kufanya maamuzi kwa sababu hawataki kuwajibika pale mambo yanapokwenda tofauti.
Hawataki lawama kama mambo yataharibika.
Hivyo wengi wanaishia kutoa mapendekezo ambayo hayawawajibishi sana.
Asante sana.
LikeLike
Kabisa, na hilo linawakwamisha sana.
LikeLike
“Kwenye haya maisha, unapaswa kufanya maamuzi au utafanyiwa maamuzi.
Unapaswa kujituma la sivyo utatumwa.
Na unapaswa kuwa na malengo yako ambayo unayapambania, la sivyo utatumika kupambania malengo ya wengine.“
LikeLike
Ndiyo hivyo, tupambane la sivyo tutapambanishwa.
LikeLike
Kwenye haya maisha ninapaswa kufanya maamuzi au nitafanyiwa maamuzi. Ninapaswa kujituma lasivyo nitatumwa. Na ninapaswa kuwa na malengo yangu ambayo ninayapambania la sivyo nitatumika kupambanaia malengo ya wengine.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Kwenye haya maisha usipofanya maamuzi utafanyiwa maamuzi,nikakumbuka pia “usipojiongoza wengine watakuongoza.
Asante sana kocha hebu tupambane kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati sahihi
LikeLike
Hakika
LikeLike