💯KCM2324082; Kuzoea.
Tumejipata, Tunaachilia Breki.
#IjumaaYaMawasiliano
Mwanamafanikio,
Mwaka wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kufanyia kazi kwa ukubwa kitu kimoja mpaka kitupe mafanikio makubwa tunayoyataka.
Tumeachilia breki kwa kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kujipa uhakika wa kufanya makubwa.

💯 Neno la leo; Kuzoea.
Leo ikiwa ni #IjumaaYaMawasiliano tunaona jinsi ambavyo kuzoea kufanya kitu tunakichukulia ni rahisi na kushindwa kubobea zaidi.
Pale ambapo tunakuwa tunafanya kitu kwa kurudia rudia, huwa tunazoea na kuweza kufanya bila hata ya kufikiri.
Hiyo ni kwa sababu akili isiyofikiri inakikariri kitu jinsi kilivyo na pale inapojitajika kukifanya, inarejea kwenye kumbukumbu hizo.
Hilo ni jambo linaloweza kuonekana la manufaa, kwa sababu mtu anaokoa muda na nguvu za kufikiri upya kila kitu.
Lakini ukweli ni kwamba kuzoea kufanya kitu siyo tu kunakuzuia kuwa bora, bali pia kunapelekea uwe mbovu kwenye maeneo hayo ambayo una mazoea nayo.
Mambo ambayo tunayafanya kila siku ndiyo ambayo huwa tunakuwa ni wabovu sana kwenye kuyafanya.
Moja ya mambo hayo ni mawasiliano yetu na watu wengine.
Kwa kuwa tunaongea na kuandika kila siku, tunadhani tayari tuko vizuri.
Lakini uhalisia ni kinyume kabisa na vile wengi tunavyodhani.
Mawasiliano yetu na wengine yanakuwa magumu pale tunapoyafanya kwa mazoea.
Kuongea pale tunapotaka kufanya hivyo na kufanya kama ulivyozoea kufanya kunapelekea ushawishi kuwa mdogo.
Ili kuwa na ushawishi mzuri, mtu unapaswa kujiendeleza kwenye eneo la mawasiliano kwa kuendelea kuwa bora.
Hivyo pia ndivyo inavyopaswa kuwa kwenye maeneo mengine yote ya maisha yako.
Kwa sababu umezoea kufanya haimaanishi unafanya kwa ubora.
Kufanya kwa ubora ni matokeo ya kufanya kitu kwa utofauti na upokee.
💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.
Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu kukubali kuwa kawaida. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2024/01/19/3306
Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku ya kuacha kutegemea kwenye mazoea ambayo unayo na badala yake kuendelea kuwa bora kwenye yale yote yanayokupa mafanikio unayoyataka.
Kocha.
💯