Pande mbili zinapokuwa zinaenda kwenye uwanja wa mapambano, ushindi huwa hauamuliwi ndani ya uwanja wa mapambano, bali nje ya uwanja. Ule upande unaoingia kwenye mapambano ukiwa umeazimia kupata ushindi pekee na siyo kingine chochote ndiyo unaopata ushindi.

Hiyo ina maana kwamba ushindi huwa unaanzia kwenye fikra na mtazamo kabla ya kudhihirika kwa nje. Wengi sana wameshindwa kupata ushindi kwenye maisha yao siyo kwa sababu hawaweki juhudi, bali kwa sababu hawajawa na mtazamo sahihi wa kuwapa ushindi.

Kitabu cha THINK AND GROW RICH kilichoandikwa na Napoleon Hill kimekuwa ndiyo msingi mkuu wa mafunzo ya maendeleo binafsi na mafanikio. Kitabu hicho kimetokana na utafiti uliofanywa na mwandishi kwa kuwahoji watu zaidi ya 500 waliokuwa na mafanikio makubwa. Kupitia watu hao aliweza kuona vitu vinavyojirudia rudia kwa karibu wote.

Aliweza kutengeneza kanuni ya mafanikio yenye misingi 13 ambayo ina nguvu ya kumpa mtu yeyote mafanikio makubwa. Mtu yeyote anayefanyia kazi misingi hiyo 13, anakuwa na uwezo wa kupata mafanikio makubwa anayokuwa anayataka.

Hiki ni kitabu ambacho sehemu kubwa ya huduma za mafunzo na ukocha ninazotoa zimejengeka kwa msingi wake. Ndoto kubwa nilizonazo, kuwa bilionea na kuwa raisi, nina uhakika wa kuzifikia bila shaka. Uhakika huu niliupata baada ya kusoma kitabu hiki cha THINK AND GROW RICH na kuanza kukiishi. Pia huduma za mafunzo, ukocha na uwajibikaji ambazo nazitoa, msingi wake ni kutoka kwenye kitabu hicho.

Hivyo naweza kusema, bila ya shaka yoyote kwamba hiki ni kitabu ambacho kila mtu aliye makini na maisha yake anapaswa kukisoma na kukiishi. Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA nimeeleza misingi hiyo 13 ya kitabu cha THINK AND GROW RICH. Sikiliza kipindi hapo hichi, jifunze na nenda kaweke kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa na kwa uhakika.

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

0678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 2. KISIMA CHA MAARIFA, 3. CHUO CHA MAUZO na 4. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.