Kwenye hizi zama za maarifa na taarifa, teknolojia ya usambaaji wa maarifa imekuwa kubwa sana. Ukiangalia ya kijamii na simu janja (smartphone) tunazotumia, ni vitu vinavyochukua sehemu kubwa ya maisha yetu.

Teknolojia hizi mpya zimekuwa zinalaumiwa kuwa chanzo cha watu kupoteza muda na maisha yao. Mfano uraibu wa mitandao ya kijamii ambapo watu wanajikuta wakipoteze muda mwingi kwenye mitandao hiyo, limekuwa ni tatizo.

Ambacho watu hawaelewi ni kwamba tatizo la muda halijatokana na hizi teknolojia mpya zilizopo, bali tatizo la muda linaanza na asili yetu sisi binadamu. Na moja ya asili yetu binadamu ni kutumia vibaya kitu chochote ambacho tunakipata bure bila ya gharama yoyote.

Kwa sababu mtu akiamka anakuwa na masaa ya siku nzima bure mbele yake, basi anajikuta akiyapoteza kwa mambo yasiyo na tija. Na hata pale anapokuwa na mambo yenye tija, huwa haoni shida kuyapeleka kesho, kwa sababu ameshazoea kesho atapata tena muda mwingine wa bure.

Ndiyo maana watu wengi wanapojikuta kwenye hali ambayo hawana tena muda wa bure, huwa wanafanya makubwa sana ndani ya muda mfupi.

Kuonyesha kwamba changamoto ya muda siyo kitu kigeni au kilicholetwa na teknolojia, miaka zaidi ya elfu 2 iliyopita, mwanafalsafa wa Ustoa aliyeitwa Seneca aliandika insha kuhusu muda. Insha hiyo aliita; ON THE SHORTNESS OF LIFE. Dhana kubwa anayoeleza kwenye insha hiyo ni kwamba muda siyo mchache, bali ni mwingi, tatizo ni watu wanaupoteza.

Sasa basi, changamoto za muda ambazo Seneca amezielezea kwenye insha hiyo ndiyo hizo hizo ambazo tunazo mpaka leo. Yaani tunateseka na mambo ambayo majibu yake yalishatolewa miaka mingi sana iliyopita.

Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA, nimeeleza kwa kina jinsi ya kutumia falsafa ya Ustoa na dhana hiyo ya Seneca kuwa na matumizi mazuri ya muda wetu na kuweza kufanya makubwa. Karibu ujifunze kwa kusikiliza kipindi hapo chini.

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

0678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 2. KISIMA CHA MAARIFA, 3. CHUO CHA MAUZO na 4. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.