Ukiiangalia punje moja ya mhindi, unaweza kuidharau na kuona ni kitu kidogo sana. Lakini punje hiyo inapopandwa kwenye ardhi yenye rutuba, inaweza kuzalisha punje nyingine nyingi sana.
Hivyo ndivyo ilivyo kwa kila kiumbe hai, kinakuwa na uwezo mkubwa ndani yake ambao hauonekani kwa nje. Hata wewe pia, ndani yako una uwezo mkubwa sana, uwezo ambao bado hujaweza kuutumia vizuri.

Kinachokukwamisha wewe kutumia uwezo mkubwa ulio ndani yako na kunufaika nao ni breki ambazo umekuwa unajiwekea wewe mwenyewe. Kwa bahati mbaya sana, huzioni hizo kama breki, bali unaziona ni maisha ya kawaida.
Bila ya kuzijua breki zinazokuzuia kutumia uwezo wako mkubwa na kuziachilia, utaondoka hapa duniani ukiwa hujatumia kabisa uwezo wako mkubwa.
Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA nimeeleza kwa kina breki zinazokuzuia wewe kutumia uwezo wako mkubwa. Nimekuonyesha maeneo manne yanayokujenga wewe kama mtu na yaliyobeba uwezo wako mkubwa.
Karibu usikilize kipindi hiki ili usiendelee kujizuia wewe mwenyewe kufanya makubwa kwenye maisha yako.
Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
0678 977 007 / amakirita@gmail.com
MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 2. KISIMA CHA MAARIFA, 3. CHUO CHA MAUZO na 4. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.