Nimekuwa nakuambia unahitaji vitu viwili tu ili uweze kujenga mafanikio makubwa sana kwenye maisha yako. Vitu hivyo ni ujifunze kuliko wengine wote na ufanye kazi kuliko wengine wote. Vitu hivyo vina nguvu ya kukupa mafanikio makubwa, lakini peke yake havitoshelezi.

Kwani wewe mwenyewe utakuwa ni shahidi wa watu wengi unaowajua ambao wamesoma sana, elimu ya darasani na hata kusoma vitabu vya mafanikio, lakini bado hawana mafanikio. Pia unawajua watu wanaofanya kazi sana, usiku na mchana lakini bado hawana mafanikio.

Hiyo ni kwa sababu licha ya kupata maarifa na kuweka kazi, kuna namna hayo yanapaswa kufanyika ili yawe na tija. Kupata maarifa na kuyafurahia haitaweza kuleta mabadiliko kwenye maisha ya mtu. Kadhalika kufanya kazi kwa namna ile ile wakati wote, haitaweza kumwinua mtu.

Kuna namna ya kujifunza na ufanyaji ambayo wale waliofanikiwa sana wamekuwa wanaitumia. Yale wanayojifunza yanakuwa na manufaa makubwa kwao. Na juhudi za kazi wanazoweka zinawapa matokeo makubwa na ya tofauti.

Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA nimeelezea namna hiyo ya kujifunza na ufanyaji inayokuwezesha kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako. Karibu ujifunze namna hiyo kwa kusikiliza kipindi hapo chini.

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

0678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 2. KISIMA CHA MAARIFA, 3. CHUO CHA MAUZO na 4. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.