💯KCM2324087; Isiyowezekana.
Tumejipata, Tunaachilia Breki.
#JumatanoYaUwajibikaji
Mwanamafanikio,
Mwaka wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kufanyia kazi kwa ukubwa kitu kimoja mpaka kitupe mafanikio makubwa tunayoyataka.
Tumeachilia breki kwa kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kujipa uhakika wa kufanya makubwa.

💯 Neno la leo; Isiyowezekana.
Leo ikiwa ni #JumatanoYaUwajibikaji tunaona jinsi ambavyo kusema maamuzi ni magumu na yasiyowezekana ni kukwepa uwajibikaji.
Kwenye maisha, huwa kuna maamuzi mbalimbali ambayo huwa tunapaswa kuyafanya.
Kadiri maamuzi hayo yanavyokuwa muhimu, ndivyo pia yanavyokuwa magumu.
Na maamuzi hayo yanakuwa magumu kwa sababu matokeo yake yanakuwa siyo ya uhakika.
Wengi huchukulia ugumu huo wa matatizo kama ni kitu kisichowezekana.
Hivyo wanajiambia hawana namna, hawawezi kuchagua au kufanya maamuzi.
Na hapo ndipo inapodhihirika kwamba tatizo siyo ugumu au kutokuwezekana kwa maamuzi.
Bali tatizo ni kukwepa kuwajibika.
Kwa sababu hakuna uhakika wa matokeo, wengi hukwepa kufanya maamuzi hayo.
Wengi hawapendi kuwajibika pale ambapo mambo yanakwenda tofauti na inavyotarajiwa.
Lakini hivyo sivyo watu wanaofanikiwa wanavyoendesha mambo yao.
Wao huwa wanakuwa tayari kuwajibika.
Hivyo wanafanya maamuzi, licha ya kukosa uhakika na kuwa magumu.
Na kwa matokeo yoyote wanayoyapata, wanayatumia kuboresha zaidi.
Wanakubali kuwajibika kwenye matokeo yoyote wanayoyapata na hivyo kuweza kupiga hatua zaidi.
Huwezi kujenga mafanikio makubwa kama haupo tayari kuwajibika.
Huwezi kufanya makubwa na magumu kama haupo tayari kukosea.
Mambo yanaweza kuwa magumu, lakini siyo kwamba hayawezekani.
Kila kitu kinawezekana pale mtu anapokuwa tayari kuwajibika kwa matokeo yoyote yatakayopatikana.
💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.
Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu matatizo sahihi na kazi. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2024/01/24/3311
Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku ya kufanya maamuzi magumu na kuwa tayari kuwajibika kwa matokeo yoyote yatakayokuja.
Kocha.
💯