💯KCM2324088; Msuguano.
Tumejipata, Tunaachilia Breki.
#AlhamisiYaUbunifu
Mwanamafanikio,
Mwaka wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kufanyia kazi kwa ukubwa kitu kimoja mpaka kitupe mafanikio makubwa tunayoyataka.
Tumeachilia breki kwa kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kujipa uhakika wa kufanya makubwa.

💯 Neno la leo; Msuguano.
Leo ikiwa ni #AlhamisiYaUbunifu tunaona jinsi ambavyo msuguano baina ya watu huwa ndiyo chanzo cha ubunifu na mawazo mapya.
Ni pale ambapo watu wanashindwa kuelewana na mawazo yao kugongana ndiyo kunatokea fursa ya kuibuka kwa mawazo mapya na hata ubunifu wa kipekee.
Watu wengi huwa wanapenda wakubalike na watu wote kwenye mawazo yao na yale wanayofanya.
Kama hilo litatokea, basi watu watabweteka sana na kubaki kwenye mazoea.
Ni pale watu wanapopingwa na kukataliwa kwenye mawazo yao na yale wanayofanya ndiyo wanapata msukumo wa kufanya kwa utofauti ambao utaleta matokeo bora zaidi.
Hivyo ndivyo ubunifu unavyozaliwa.
Kwa mawazo mazuri na ubunifu wa kweli unahitaji ushirikiano wa watu, migogoro, mabishano na mijadala.
Hivyo ndivyo vitu vinavyochochea upatikanaji wa mawazo tofauti na ubunifu wa kipekee.
Pale unapopingwa na kukataliwa na wengine kwenye kile unachofikiria na kufanya, usiumie.
Badala yake jiulize wapi hawajaelewa na unawezaje kuwaonyesha kwa matendo na siyo maneno pekee.
Hilo litakusukuma uwe na ubunifu wa tofauti na ambao utaleta matokeo bora.
Tutengeneze misuguano chanya kwa timu tunazoshirikiana nazo ili tuweze kutoa fursa ya kuzaliwa kwa mawazo mapya na kuleta ubunifu wa kipekee.
💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.
Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu hatua na matokeo. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2024/01/25/3312
Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku ya kutumia misuguano kama fursa ya kuja na mawazo mapya na ubunifu wa kipekee.
Kocha.
💯