Mpendwa muuzaji bora kuwahi kutokea,

Kutokukamilisha mauzo, ni ugonjwa wa wauzaji wengi. Tunajua kwamba kukamilisha mauzo ndiyo ushindi lakini tunapofika eneo la fedha ni huwa tunakua tunajizima data kama hatutaki hela.

Wote tunajua wimbo alioimba Banana Zoro unaitwa Zoba,
Msanii analalamika kwamba anajiona Zoba kwa sababu alikuwa na mpenzi wake, lakini yeye alikuwa ana ngoja ngoja, subira yake ikampoza na kuonekana Zoba, anasema kabisa, mauzo yote? Halafu sijmpata si uzoba huu?

Hata sisi wauzaji tunakua na uzoba, tunakua na mteja, tunafikiri kwamba hawezi kwenda kununua sehemu nyingine, badala ya kumwambia alipie tunaanza kujizungusha mpaka mteja anaacha kununua.
Usikubali kuwa zoba, kamilisha mauzo. Ushindi wako ni faida na faida inapatikana kwa wewe kuuza tu.

Ni jambo la kushangaza, lakini watu wengi hukaa kwenye mchakato mzima wa mauzo, kuwaeleza wateja kuhusu kile wanachouza, lakini wanapofika mwisho hawajaribu kukamilisha mauzo. Yaani wanafika mwisho halafu wanategemea wateja waamue wenyewe kufanya maamuzi ya kununua. Wanachopata ni sababu na ahadi hewa na kuwapoteza wateja hao.

Watu wengi husita kuwaambia wateja wanunue kwa kuhofia kuambiwa hapana. Lakini kinachotokea ni kupata hapana iliyo kubwa, maana wateja hawanunui kama hawajaambiwa wanunue.

Kwenye mchakato wako mzima wa mauzo, hakikisha unawaambia wateja wanunue na unawasisitizia hilo. Huwezi kukamilisha mauzo kama hutawaambia wateja wanunue.
Usikubali kupoteza mauzo yako na kuonekana Zoba.

Habari njema ni kwamba, leo tunaendelea na mbinu za ukamilishaji wa mauzo na leo ni namba 15 na 16.

17. Ukamilishaji wa kukubaliana – 1.
Unamwambia mteja “Nakubaliana na wewe ni fedha nyingi, nahitaji uweke sahihi yako hapa au tukamilishe mauzo.

Mteja anakuambia ni fedha nyingi, wewe unamwambia nakubaliana na wewe ni fedha nyingi tukamilishe mauzo.

Kukubaliana na mteja ni sheria muhimu ya ukamilishaji. Unachofanya hapa ni kukubaliana naye lakini kutoruhusu sababu yake kuwa kikwazo. Kwa kuwa umeshakubaliana naye, anakuwa hana cha kubishana tena bali ni kumwambia tu akamilishe malipo.

18. Ukamilishaji wa kukubaliana – 2. “Nakubaliana na wewe ni fedha nyingi, na nategemea ulijua hilo kabla hujaja hapa. Nahitaji uweke sahihi yako hapa au tukamilishe hili, ”

Watu huwa wanajua bei ni kubwa kabla hata hawajaja, lakini wanakuja, kwa sababu wana uhitaji. Kamilisha mauzo, hakuna mtu amewahi kusema nimependa bei yako, kila mtu hulalamikia bei kabla ya kukamalisha, kubaliana nao kisha kamilisha mauzo.

Hatua ya kuchukua leo; Nenda kakamilishe mauzo na usikubaliane na sababu anazokupa mteja.

Kitu kimoja zaidi kwenye mauzo, acha chenga nyingi, ukipata nafasi ya kushinda goli SHINDA. Ukiona mteja tayari ameshaonea kukubali kitu, kamilisha mauzo mara moja bila kusubiri na kujizungusha mpaka mteja anaacha kununua.

Kauli mbiu yetu ni ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA.

Kutoka kwa muuzaji mwenzako, rafiki anayekupenda na kukujali,

Mwl.Deogratius Kessy

Mwalimu/Mwandishi/Mkufunzi wa mauzo.
Makamu Mkuu wa CHUO CHA MAUZO.
makamu@mauzo.tz