
Kuna gari iligoma kuwaka kwa miezi kadhaa. Kila fundi aliyejaribu
kuitengeneza alitoka kapa. Mwenye gari akasikia kuna fundi sehemu fulani anaweza kumaliza tatizo lake. Akamfuata na kumleta katika “garage” yake. Fundi huyo alifika na kuanza kuichunguza gari kuanzia juu hadi chini. Huku akifungua na kuwasha mara kadhaa.
Baada ya hapo akafungua sehemu ya mafuta, na sehemu zingine, kisha akachukua nyundo yake, akagongagonga juu ya injini na kumwambia mwenye gari aingie na kuwasha.
Mzee Juma kuwasha tu, gari likawaka. Akaruka kwa furaha, maana hakuamini kama lile zoezi la kugongagonga injini ndani ya sekunde chache lingewasha gari.
Mzee Juma akamuuliza, sasa fundi hapa nikulipe kweli? Maana ni nyundo tatu tu umepiga. Fundi Rashid akamwambia, ninapaswa kulipwa na gharama zote ni laki tano.
Mzee Juma akasema, yaani kugonga tu na nyundo ndio unataka laki tano? Fundi Rashid akauuliza, mafundi wangapi wamekuja hapa na kushindwa? Mzee Juma akasema ni zaidi ya tano.
Fundi Rashid akasema, umeonae? Kumbe, napaswa kulipwa. Na hulipi nyundo nilizopiga bali akili, niliyotumia kufikiria na kuleta suluhu juu ya gari lako. Mzee Juma akainama chini, kisha akalipa.
Kwa hiyo unaweza kuona namna gani, kuijua biashara yako kwa kina kunavyokusaidia kutatua haraka juu ya tatizo lolote linalojitokeza pamoja na kuokoa muda.
Umuhimu Wa kujua biashara Kwa kina;
Moja; Kuokoa Muda.
Mfano mzuri, tumeona kwa fundi Rashid. Amefanya uchunguzi kwanza na kujua sehemu sahihi yenye tatizo.
Mbili; Kaminika.
Watu hununua kwa watu wanaowaamini na kuwapenda. Hii inatokana na suluhu wanayopata kutoka kwao.
Tatu; Kujua wapi nguvu itumike na akili pia. Ndiyo maana ninasema, “nguvu nyingi huenda akili isipofika” Wakati “akili huenda pesa isipofika”.
Nne; Kujibu Mapingamizi.
Wateja hawana subira, jambo dogo linapotokea wanalalamika. Ikiwa unaijua biashara yako kwa kina inakusaidia kumwelezea mteja kwa ukubwa.
Hatua za kuchukua leo; Tenga muda wa kujifunza zaidi na kujua biashara yako kwa kina. Hii ni kwa sababu ukiijua biashara yako, utawavutia zaidi wateja wako.
Soma pia; https://atomic-temporary-134799883.wpcomstaging.com/2024/02/29/uaminifu-ni-salio-lisilo-na-ukomo/
Imeandaliwa na Lackius Robert Mkufunzi Msaidizi Chuo Cha Mauzo na Mwandishi. Tuwasiliane 0767702659 au mkufunzi@mauzo.tz.