Rafiki yangu mpendwa,

Watu huwa wanalalamika kwamba umasikini unawazuia kuishi maisha ambayo wangetaka kuyaishi. Wanaona kama vile umasikini unawang’ang’ania na hautaki kabisa kuwaachia.

Lakini hilo mimi nimekuwa nalikataa. Ukweli ni kwamba, watu ndiyo wanaung’ang’ania umasikini kuliko umasikini unavyowang’ang’ania wao. Watu wanaukumbatia umasikini na kuhakikisha hauwatoki kabisa.

Unaweza kujiuliza ni kwa nini watu wakumbatie kitu ambacho kinawatesa? Na jibu lipo wazi, inawaondolea uwajibikaji. Mtu akilalamikia umasikini, anasikilizwa na kuonewa huruma. Lakini mtu akiukataa umasikini, inabidi apambane kuonyesha kweli kamba anafanya makubwa. Kwa kuwa watu hawataki kupambana, basi wanaishia kuukumbatia umasikini ili wasiwajibike.

Kuna njia nyingi ambazo watu wamekuwa wanazitumia kuukumbatia umasikini. Njia moja, ambao imekuwa na nguvu na kuwaathiri wengi ni kauli ambazo watu wamekuwa wanazitumia.

Kuna kauli ambazo watu wamezuia kuzitumia na kuona kama ni za kawaida, ila ni kauli ambazo zimekuwa zinahalalisha sana umasikini kwao. Kwa mtu kutumia kauli hizo anakuwa anaona umasikini ni kitu sawa kabisa kwake. Kama watu hawataacha kutumia kauli hizo, hawataweza kupambana na umasikini.

Umasikini ni kitu ambacho kinapaswa kupigwa vita vikali sana na mtu yeyote anayetaka kuachana nao. Siyo kitu cha kuchekewa wala cha lele mama. Ni adui ambaye ana kila aina ya silaha za kukutawala, bila ya wewe kujua. Hivyo kumwendea kwa upole ni kuzidi kumpa nguvu.

Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA nimeshirikisha kauli za kufulia ambazo wengi wanapenda kuzitumia na zinawaweka kwenye umasikini. Najua hata wewe umezizoea sana kauli hizi na zimekuwa zinakukwamisha. Karibu uangalie kipindi ili uachane na kauli hizo mara moja na uweze kutoka kwenye umasikini kabisa.

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

0678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.