3361; Hofu na kulazimisha.

Kutoka mezani kwa Kocha,

Rafiki yangu mpendwa,
Kupata au kukosa yale tunayotaka, huwa hakutokani sana na hatua tunazochukua au kushindwa kuchukua. Bali kunategemea zaidi mtazamo ambao tunakuwa nao.

Kadiri unavyokuwa unalazimisha kukipata kitu, ndivyo unavyozidi kukikosa. Kupitia kulazimisha kwako, unajikuta ukifanya makosa ambayo yanazidi kukukosesha yale unayotaka.

Yale unayokuwa unayahofia ndiyo unayoyakaribisha kwenye maisha yako. Unapokuwa unakihofia kitu, unajikuta unakifikiria kwa muda mrefu. Na kile unachokifikiria kwa muda mrefu akili yako inakiona ndiyo muhimu na hivyo kuleta fura zinazoendana na hicho.

Kwa maana hiyo basi, kupata unachotaka, jua kile unachotaka, kifikirie na kukifanya muda wote na uwe na subira.
Kufanya yale yaliyo sahihi na kujipa muda ni njia ya uhakika ya kupata kile unachotaka.

Kwenye jamii ya KISIMA CHA MAARIFA, ambayo ni jamii ya tofauti tunayoijenga, mara zote tumejipanga vizuri kuhakikisha tunapata kile tunachotaka.
Mara zote tunafikiria kile tunachotaka kwa kila siku kuyaandika malengo makubwa tuliyonayo.
Na pia tunajipa muda wa kutosha wa kuyafanyia kazi malengo hayo makubwa bila ya kuyapoteza kwa kulazimisha.

Ndani ya jamii ya KISIMA CHA MAARIFA, hakuna kuchelewa. Tunajua kila kitu kina sababu za kuwepo kwa wakati wake na tunakwenda na kila kitu kwa namna hiyo.
Tunageuza hofu kuwa fikra za kujirudia rudia kwa wakati wetu wote na hizo ndiyo zinatawala akili zetu.
Tunageuza kulazimisha kuwa mchakato ambao tunaufuata mara zote bila ya kuacha.

Kupata unachotaka, kuna mengi yanayohusika zaidi ya kile unachofanya.
Yazingatie hayo ili uweze kupata yale unyoyataka mara zote.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe