Rafiki yangu mpendwa,

Kanuni ya asili huwa inafanya kazi kwa kuzalisha vitu kwa wingi kuliko vinavyohitajika. Ni kupitia wingi huo ndiyo kumekuwa na uhakika wa vile vitu vinavyokuwa vinahitajika sana.

Lakini sisi binadamu, kwa sababu ya maono madogo tunayokuwa nayo, tumekuwa tunahangaika na kuwa na pungufu kwenye vitu vyote muhimu tunavyokuwa navyo.

Watu wengi wanataka wafanye kazi kidogo na kupata kipato kikubwa.

Watu wengi wanaishia kuwa na kipato kidogo kuliko wanavyohitaji, huku wakijifariji kwamba wanaridhika nacho. Lakini ukweli ni kwamba hakuna namna mtu anaweza kuishi maisha ya kuridhika kama ana kipato ambacho hakitoshelezi mahitaji yake.

Hebu fikiria kama bahari ingekuwa na samaki pungufu kuliko mahitaji ya watu, je leo hii kungekuwa na samaki? Mpaka leo kuna samaki kwa sababu bahari huwa inazalisha kwa wingi kuliko mahitaji.

Ukiangalia hata mwili wako, una vitu vingi vya ziada kuliko inavyohitajika. Kwa mfano mtu akiwa na figo moja inatosha kufanya kazi ya mwili mzima. Lakini mtu mwenye afya kamili huwa ana figo mbili, hiyo ni zaidi ya unavyohitaji. Kwa kuwa na figo mbili, hata moja ikipata changamoto, nyingine inaendelea kufanya kazi na maisha yanaendelea.

Kanuni ya furaha kwenye maisha huwa ni uhalisia gawanya kwa matarajio. Uhalisia ukiwa ni matokeo unayopata na matarajio ikiwa ni mahitaji unayokuwa nayo. Hiyo ina maana kwamba kama ukiweza kuzalisha matokeo ya ziada kuliko mahitaji yako, utaongeza furaha yako.

Karibu kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ujifunze jinsi unavyoweza kuwa na ziada kwenye kila eneo la maisha yako ili kuwa na furaha. Fungua kipindi hapo chini kujifunza.

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

0678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.