Habari njema muuzaji bora kabisa kuwahi kutokea,

Karibu sana kwenye mwendelezo wa makala zetu za ukamilishaji ambazo ni mwendelezo wa makala kutoka CHUO CHA MAUZO.

Hongera sana kwa kuendelea kujifunza na kuchukua hatua kwa haya unayoendelea kujifunza hapa.

Leo ni jumatano ya ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA.

Kama kauli mbiu inavyosema, mara zote unapaswa kukamilisha wateja na wewe pia unapaswa kukamilisha wateja. Na kukamilisha ndiyo wajibu wako namba moja kwenye biashara yako.
Wajibu wako namba moja ni kuuza na unapokuwa umemuuzia mteja maana yake umemkamilisha.
Hivyo basi, kila wakati wageuze wateja tarajiwa uliokuwa nao na waweze kununua na kuwa wateja kamili.

Ukamilishaji ndiyo kitu muhimu sana kwenye mauzo kwa sababu ndiyo kitu pekee kinacholeta kinaleta ushindi kupitia kile unachouza iwe ni bidhaa au huduma.

Kumkamilisha mteja inahitaji sanaa na sayansi ya kuwa muuzaji bora kuwahi kutokea. Na kwa kuwa kwenye CHUO CHA MAUZO na pamoja na kitabu chetu cha mwongozo wa program, yaani kitabu cha CHUO CHA MAUZO, tunajifunza sanaa na sayansi ya kuwa muuzaji bora kuwahi kutokea.

Wewe kama muuzaji bora kabisa kuwahi kutokea, unatakiwa kuwakamilisha wateja na kuwauzia kile unachouza kwa sababu una kitu kizuri na kina manufaa kwao na huuzi kitu haramu au madawa ya kulya ni wajibu wako kabisa wa kimaadili kumshawishi mtu kununua kile unachouza.
Kila wakati jiambie, usiposhika hela ya mteja maana yake mteja amekuuzia na wewe hauko hapo kwa ajili ya kuuziwa bali kuuza.

Kwenye somo letu lililopita tulijifunza mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo nayo ni mbinu namba 25 na 26.
Kwenye mbinu namba 25 tulijifunza ukamilishaji wa bidhaa ya juu. Na kwenye ukamilishaji wa namba 27 ulijifunza ukamilishaji wa bidhaa mbadala.
Kama ulienda kuzifanyia kazi na kupata matokeo basi karibu sana utushirikishe namna ulivyonufaika nazo mbinu hizo.

SOMA; Mbinu Mbili Za Uhakika Za Ukamilishaji Wa Mauzo 25-26

Leo kwenye ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu yetu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA, tunakwenda kujifunza mbinu nyingine mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo nazo ni mbinu namba 27 na 28

Zifuatazo ni mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo ambazo tunakwenda kujifunza hapa;

  1. Ukamilishaji wa kupunguza kifurushi

Mara zote mwonyeshe mteja njia ya kupata kile anachotaka.

Kama kifurushi kina vitu vingi ambavyo huenda hatatumia, unaweza kuvipunguza na akaweza kumudu bei.

Kwa mfano, mteja amekuja kwako na anataka bidhaa au huduma fulani unayotoa, na unaona analalamika kuhusu kifurushi ni kikubwa, unaweza kumpunguzia kifurushi ili aweze kumudu bei na kununua kile unachouza iwe ni bidhaa au huduma.

Unamwambia mteja,
“Kama hutaki kuchukua ya chini au tofauti, kwa nini usipunguze kifurushi? Utapunguza baadhi ya vitu, lakini utapata ubora ule ule kwa bei ya chini kidogo.

Lengo la ukamilishaji huu, ni mteja asiondoke bila kuchukua kitu, kama vitu anavyotaka ni vingi, mpunguzie vitu ili apate gharama inayoendana na kiasi alichokuwa nacho.

  1. Ukamilishaji wa kugawa malipo.

Unatumia ukamilishaji huu pale kile unachouza kinapokuwa na vitu vya ziada ambayo bei yake ni tofauti na kitu halisi.

Mfano gari ambalo lina vitu vya ziada vinavyofanya bei iwe juu, lakini ukiviondoa, bei halisi ya gari inakuwa siyo kubwa kwa mteja.

Au huduma ya ujenzi, gharama inaweza kuwa kubwa kama ukijumlishia kila kitu kwenye bei lakini ukitoa vitu vingine na kuacha gharama halisi la labda ya ramani tu ya jengo inakuwa ndogo kuliko pale unapomwambie mteja gharama ambayo inajumuiya kwenda kutembelea na kuona eneo, ushauri wa kitaalamu, vibali halmashauri nakadhalika.
Kwa mfano unamwambia mteja,
“Ukiondoa vitu vya ziada, malipo halisi unayolipa ni kiasi hiki…. ambayo iko ndani ya bajeti uliyosema. Unaweza kuchukua bila ya vitu hivyo vya ziada, au ukachukua hivyo vya ziada kwa mpango mwingine.”

Kitu kikubwa cha kuondoka nacho hapa wewe kama muuzaji ni kwenda kutumia haya maarifa uliyopata hapa na kumshawishi mteja kuchukua hatua ya kununua licha ya vipingamizi ambavyo anakuletea.
Usikubali mteja kukupiga chenga wakati wewe tayari una silaha 28 za ukamilishaji wa mauzo. Zitumie kupata ushindi na kumbuka wewe kazi yako ni kuuza na mara zote unapaswa kukamilisha wateja.

Kutoka kwa muuzaji mwenzako, rafiki anayekupenda na kukujali,

Mwl.Deogratius Kessy

Mwalimu/Mwandishi/Mkufunzi wa mauzo.
Makamu Mkuu wa CHUO CHA MAUZO.
makamu@mauzo.tz