Habari njema muuzaji bora kabisa kuwahi kutokea,

Karibu sana kwenye mwendelezo wa makala zetu za ukamilishaji ambazo ni mwendelezo wa makala kutoka CHUO CHA MAUZO.

Hongera sana kwa kuendelea kujifunza na kuchukua hatua kwa haya unayoendelea kujifunza hapa.

Leo ni jumatano ya ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA.

Kama kauli mbiu inavyosema, mara zote unapaswa kukamilisha wateja na wewe pia unapaswa kukamilisha wateja. Na kukamilisha ndiyo wajibu wako namba moja kwenye biashara yako.
Wajibu wako namba moja ni kuuza na unapokuwa umemuuzia mteja maana yake umemkamilisha.
Hivyo basi, kila wakati wageuze wateja tarajiwa uliokuwa nao na waweze kununua na kuwa wateja kamili.

Ukamilishaji ndiyo kitu muhimu sana kwenye mauzo kwa sababu ndiyo kitu pekee kinacholeta fedha kwenye biashara kupitia kile unachouza iwe ni bidhaa au huduma.

Kwenye somo letu lililopita tulijifunza mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo nayo ni mbinu namba 27 na 28.
Kwenye mbinu namba 27 tulijifunza ukamilishaji wa kupunguza kifurushi.
Na kwenye ukamilishaji wa namba 28 ulijifunza ukamilishaji wa kugawa malipo.
Kama ulienda kuzifanyia kazi na kupata matokeo basi karibu sana utushirikishe namna ulivyonufaika nazo mbinu hizo.

SOMA; Mbinu Mbili Za Uhakika Za Ukamilishaji Wa Mauzo 27-28

Leo kwenye ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu yetu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA, tunakwenda kujifunza mbinu nyingine mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo nazo ni mbinu namba 29 na 30.

Zifuatazo ni mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo ambazo tunakwenda kujifunza hapa;

29.Ukamilishaji wa bajeti – 1.

Pale mteja anaposema yupo juu ya bajeti.
Mwambie hivi,
“Kila mteja anayenunua hapa huwa anakuwa juu ya bajeti, lakini huwa wanakamilisha hilo. Nahitaji uweke sahihi yako hapa, nahitaji tukamilishe hili, nahitaji ulipie sasa, ipi njia nzuri ya kukamilisha malipo?

Mpendwa muuzaji bora kuwahi kutokea, mtu anakuwa yupo juu ya bajeti kwa sababu amenunua vitu, hivyo usisite kumuuzia, atanunua pia.

Hata kama hatanunua, bado yupo juu ya bajeti, hivyo hakikisha unakamilisha mauzo.
Kwa sababu, wateja wengi wanasema hivyo wako juu ya bajeti siyo kwamba hawana hela, wanayo wanachotaka ni wewe uweze kugusa maumivu yao na kuyatumia maumivu hayo kuwakamilisha.

30. Ukamilishaji wa bajeti – 2.

Mteja anakuambia tena pingamizi la bajeti, wewe unamwambia;
“Tayari kuna vitu vingine unavyolipia juu ya bajeti, kama gari, bima, kodi, umeme na mahitaji muhimu.
Yote hayo unalipia juu kuliko unavyotaka, lakini huna budi bali kulipia. Nahitaji uweke sahihi yako hapa, nahitaji tukamilishe hili, nahitaji ulipie sasa ili uende ukafurahie uwekezaji wako, nahitaji tukamilishe kwa sababu ni hitaji muhimu kwako.

Punguza nguvu ya pingamizi lake la bajeti kwa kuonyesha ni kitu cha kawaida ambacho tayari anafanya, kisha kamilisha mauzo.

Hatua ya kuchukua leo; waoneshe wateja kwamba mapingamizi wanayokupa ya bajeti ni mahitaji muhimu ambayo wanayafanya kila siku ya kuwa juu ya bajeti. Lakini, waambie hawana budi bali kulipia tu.

Kwa namna yoyote ile, hakikisha unatumia mbinu 30 ambazo tumefikisha leo kukamilisha mauzo.
Angalia ni mbinu gani kati ya hizi ulizojifunza ambazo zinaendana na pingamizi ambalo mteja amekupa na kisha tumia kukamilisha mauzo.
Hizi ni silaha za mauzo, na mauzo ni vita isiyoruhusu umwagaji damu, tumia silaha hizi pale unapokutana na wateja ambao wana mapingamizi mbalimbali wanayokuwa nayo na kisha kuwauzia.

Kutoka kwa muuzaji mwenzako, rafiki anayekupenda na kukujali,

Mwl.Deogratius Kessy

Mwalimu/Mwandishi/Mkufunzi wa mauzo.
Makamu Mkuu wa CHUO CHA MAUZO.
makamu@mauzo.tz