Rafiki yangu mpendwa,
Kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 ambapo nimekuwa nafundisha na kushauri mafanikio, nimekutana na watu wengi wanaokuja wakiomba ushauri.
Mtu anaomba ushauri kwamba ana kiasi cha fedha, milioni 20 na hajui biashara gani afanye. Anakuwa anataka ushauri wa biashara anayoweza kufanya kwa mtaji huo na ikamlipa vizuri.
Falsafa yangu kwenye ushauri ni ushauri wa mara moja huwa haufanyi kazi. Yaani uambiwe tu kafanye biashara fulani na itakulipa, haiwezi kuwa rahisi hivyo. Hivyo basi, huwa namtaka mtu ajifunze kwanza misingi ya biashara. Na hapo ndiyo namwambia kwanza apate na kusoma kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA.

Wengi wakishasikia swala la kusoma kitabu cha biashara, wanaona hawawezi. Wao wanachotaka ni kusikia tu neno wakafanye biashara gani itakayowalipa. Hivyo wanapuuza na kwenda kutafuta ambapo watapewa maneno matamu ya kuwafurahisha.
Kwa sababu watu huwa ni rahisi sana kutoa ushauri, basi wenye mitaji huwa wanaishia kupewa ushauri wa biashara za kuanzisha ambazo zitawalipa haraka. Wanaingia kwa tamaa ya kupata mafanikio ya haraka, tena bila ya kuweka kazi kubwa.
Matokeo huwa ni kilio, kwani wanaishia kupoteza mtaji wote waliokuwa nao na hakuna biashara wanayobaki nayo. Hayo yanakuwa ni maumivu makubwa sana ambayo yamesababishwa na uzembe wa mtu mwenyewe, kwa ukaidi wake wa kujifunza.
Huwa kuna kauli inasema; mwenye fedha akikutana na mwenye uzoefu, mwenye uzoefu anaondoka na fedha na mwenye fedha anaondoka na uzoefu. Yaani kama huna uzoefu kwenye jambo lolote lile, utaishia kulipa gharama kubwa sana kuupata huo uzoefu. Lakini kuna njia ya kupata uzoefu bila ya kuingia gharama hizo kubwa.
Njia hiyo ni kujifunza misingi ya kitu na kisha kuanza kuifanyia kazi kwa hatua ndogo ndogo huku ukiboresha kulingana na matokeo ambayo yanapatikana. Hakuna njia ya mkato kwenye hili, misingi haiwezi kuvunjwa, ni lazima isimamiwe mara zote.
Watu wengi wanakwama kwa sababu wanapuuza misingi ya kitu husika. Wanafikiri kuna njia ya mkato ya kupata matokeo makubwa bila ya kuweka juhudi kubwa. Lakini mara zote huwa wanaishia kuumia wao wenyewe.
Rafiki, kama unapanga kuanza biashara au tayari upo kwenye biashara, kuna misingi ya biashara ambayo unapaswa kuizingatia ili iweze kukua na kukupa mafanikio makubwa. Wengi sana wanaoshindwa kwenye biashara siyo kwa sababu hawana mtaji au biashara hailipi, bali ni kwa sababu hawaijui na kuizingatia misingi sahihi ya biashara.

Kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA kimeelezea misingi yote ya biashara ambayo unapaswa kuisimamia ili kujenga biashara yenye mafanikio makubwa. Ni kitabu ambacho kila mtu aliye kwenye biashara anapaswa kuwa nacho kama mwongozo wake kwenye kuiendesha biashara yake.
Kama bado hujawa na kitabu hiki, chukua hatua sasa kujipatia nakala yako. Wasiliana na namba 0678977007 kujipatia kitabu chako sasa ili uache kupoteza mtaji wako wa biashara kwa kutokujua na kuzingatia misingi ya biashara.
Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA nimekueleza baadhi ya mambo ya msingi kutoka kwenye kitabu hicho. Karibu ujifunze hayo kwenye kipindi hapo chini.
Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
0678 977 007 / amakirita@gmail.com
MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.