3410; Hakuna unayemdanganya.
Kutoka mezani kwa Kocha,
Rafiki yangu mpendwa,
Watu wote wanaokuzunguka, wanaujua ukweli kuhusu wewe.
Hata kama unajaribu kuficha ukweli wako kwa sababu mbalimbali, wale wanaokuzunguka huwa wanaujua ukweli wote kuhusu wewe.
Eneo ambalo huwa unapenda kulificha na watu wasijue ni aina ya maisha unayokuwa unayaishi.
Kwa nje unaweza kuwa na maigizo mengi ambapo unataka watu wakuoje unapenda kile unachofanya na unaweka juhudi kubwa kwenye hicho.
Lakini pale uhalisia wako unapokuwa tofauti na vile unavyoigiza, watu huwa wanaona uhalisia na kuuamini huo.
Watu wanaona kabisa kwamba huyaishi maisha yako kwa ukamilifu wake.
Watu wanaona jinsi unavyokuwa unaishi maisha yasiyo na kusudi.
Pale unapokosa kusudi kubwa la maisha yako, unajikuta ukihangaika na kila linalokuja mbele yako, kitu kinachokupoteza zaidi.
Kwa kukosa kusudi na mwelekeo wa maisha, kila mtu anakuwa na la kusema juu yako.
Kukosa kusudi na mwelekeo wa maisha kubapelekea watu;
1. Kutoa changamoto kwa mwenendo wa maisha yako.
2. Kukudanganya na kunufaka kupitia wewe.
3. Wengi hawatakuwa na matumaini makubwa kwako.
Wajibu wako namba moja kwenye maisha ni kuishi kwa ukamilifu maisha yako.
Unapaswa kwenda kwa kasi kubwa na kwa halisi, ambayo watu wataiheshimu na kutaka kwenda hivyo.
Usiigize maisha yako ili kuonekana kwa namna fulani, watu huwa wanaona nyuma ya maigizo unayokuwa unayafanya.
Kuwa mkweli kwako mwenyewe na kwa wengine ili uweze kuwavutia na kufanya kwa usahihi.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe