Rafiki yangu mpendwa,
Kila mtu ambaye yupo kwenye ajira, bila ya kujali kiasi cha mshahara anacholipwa, kimekuwa hakitoshelezi.
Kipato cha mshahara pamoja na uhakika wake wa kupatikana kila mwezi, kimekuwa ni kipato kidogo kuliko mahitaji ambayo watu wanayo.
Hivyo ndoto ya wengi ambao wapo kwenye biashara na wangependa kipato chao kiongezeke ni kufanya biashara. Wengi tayari wanajua kwamba kama wanataka kipato kikubwa na kisicho na ukomo, basi wanatakiwa kuwa na biashara.

Lakini wengi kati ya hao wanaojua wanapaswa kuanzisha biashara, bado hawajaanza biashara. Bado wanaendelea kutegemea ajira zao huku pia wakiendelea na malalamiko ya kipato kutokutosheleza.
Sababu kubwa wanayotumia ya kushindwa kuingia kwenye biashara ni kukosa mtaji. Wanaeleza wazi kabisa jinsi wanavyotaka sana kufanya biashara, ila hawana mtaji.
Wanakuonyesha jinsi kipato kidogo wanachoingiza kinavyoshindwa kuwatosheleza na hivyo kushindwa kabisa kukusanya mtaji.
Japokuwa hawapo sahihi kwenye hilo, tunaweza kukubaliana nao kwamba kweli kwa udogo wa kipato na ukubwa wa matumizi, wameshindwa kupata mtaji wa kuanza biashara.
Lakini je, vipi fursa mbalimbali ambazo zimemzunguka kila mtu, za kuweza kuongeza kipato kwa ukubwa sana bila ya kuhitaji mtaji wa aina yoyote? Je mtu anaweza kuziona na kuzitumia fursa hizo ambazo zinamzunguka?
Hicho ndiyo kitu ambacho nataka wewe rafiki yangu ukitambue na kukifanyia kazi ili uweze kutoka hapo ulipokwama sasa.
SOMA; BIASHARA NDANI YA AJIRA; Mwongozo Wa Kuanzisha Na Kukuza Biashara Yako Ukiwa Kwenye Ajira.
NJIA YA UHAKIKA YA KUINGIZA KIPATO BILA HATA YA KUWA NA MTAJI.
Rafiki, ipo njia moja ya uhakika kabisa kwako kuweza kuingiza kipato kikubwa bila ya kuwa na mtaji kabisa.
Njia hiyo haihitaji hata usumbuke na mengi ambayo unapaswa kusumbuka nayo ukiwa kwenye biashara.
Kwa mfano hutahitajika kuwa na leseni ya kufanya biashara, kuwa na namba ya mlipa kodi au eneo la biashara.
Unachohitajika kuweka wewe ni juhudi tu na moja kwa moja unaanza kuingiza kipato.
Rafiki, njia ninayozungumzia hapa ni KUFANYA MAUZO.
Kufanya mauzo ni njia ya uhakika ya kila mtu kuweza kuingiza kipato kikubwa bila ya kuwa na mtaji wowote ile.
Njia hii inafanya kazi kwa mfumo ufuatao;
1. Wewe unaangalia katika vitu ambavyo unanunua na kutumia mara kwa mara, kipi ambacho unakipenda sana na umekuwa unawapendekezea wengine nao wakinunue.
2. Watafute wale ambao wanauza kitu hicho na wape mpango wa wewe kuwa unawapelekea wateja ambao wananunua kwa uhakika na pale wanaponunua basi wao wakupe wewe kamisheni kutokana na mauzo hayo. Hapo utapendekeza njia nzuri ya kujua watu uliowaleta wewe na wakanunua.
3. Ingia kwenye kazi ya mauzo, anza kuongea na watu wengi ukiwaeleza jinsi wewe umenufaika na kitu hicho na wao wanavyoweza kunufaika pia. Kadiri unavyoongea na wengi na kutumia ushuhuda wako, huku ukiwaonyesha na wao wanavyoweza kunufaika, ndivyo utakavyopata ambao watakuwa tayari kununua.
4. Kamilisha mauzo kisha lipwa kamisheni yako kutokana na mauzo hayo. Na hapo unakuwa umeweza kuingiza kipato bila ya mtaji kabisa.
5. Huhitaji kufanya hili muda wote wa siku, unaweza kutenga hata masaa mawili tu kwa siku ya kufanya hivyo. Na unaweza kutumia njia mbalimbali, kama kukutana na watu ana kwa ana, kuwasiliana nao kwa simu au kutumia mitandao ya kijamii. Kwa njia yoyote ile, ukiweka juhudi, utaweza kupata matokeo mazuri.
Ukifanyia kazi huu mpango mfupi niliokushirikisha hapo, utaweza kuona manufaa yake kwa haraka kabisa.
Kwenye kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA, nimekuonyesha jinsi unavyoweza kukuza kipato chako kwa uhakika ukiwa bado umeajiriwa kwa kufanya mauzo. Hicho ni kitabu ambacho unapaswa kuwa nacho ili uweze kukuza kipato chako hata kama huna pa kuanzia kabisa.
Pia kitabu cha CHUO CHA MAUZO kinakupa mwongozo mzuri wa kukufanya wewe kuwa muuzaji bora, kwa kuwa na ushawishi sahihi unaowafanya watu wakubali kununua kile unachouza. Ni kitabu unachopaswa kuwa nacho kwa sababu kitakusaidia maeneo yote ya maisha yako.
Kupata vitabu hivyo, wasiliana na namba 0678 977 007.
Habari njema ni kwamba, huo mpango niliokupa hapo juu, unaweza kuanza nao kwenye vitabu hivyo. Kwa kuvipata vitabu, ukavisoma na kuvielewa, ukaona watu wengine nao wanavihitaji, washawishi wavipate na wasiliana na sisi tutakulipa kamisheni kutokana na mauzo uliyosababisha.
Rafiki, hiyo ni fursa nzuri kwako kuanza kufanyia kazi maarifa haya na ukanufaika nayo moja kwa moja. Pata kwanza kitabu, soma na elewa kisha wasiliana na namba 0678 977 007 kuweka mpango wa wewe kulipwa kwa watu unaowaleta wakanunua.
Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA hapo chini nimefafanua zaidi jinsi unavyoweza kutumia mauzo kuingiza kipato bila kuwa na mtaji. Karibu ujifunze.
Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
+255 678 977 007 / amakirita@gmail.com
MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.