3432; Hakuna kushindwa.

Kutoka mezani kwa Kocha,

Rafiki yangu mpendwa,
Kwenye safari ya mafanikio kwenye maisha, huwa kuna juhudi ambazo mtu unaweka na matokeo yanayopatikana.

Kwa haraka haraka unaweza kudhani matokeo yanayopatikana hapo ni ya aina mbili; kufanikiwa kupata unachotaka au kushindwa.
Lakini hivyo sivyo uhalisia ulivyo, kwani kwenye matokeo, huwa hakuna kushindwa.

Kwa safari yoyote ya mafanikio unayokuwepo, kuna matokeo ya aina tatu;
Moja ni kupata kile unachotaka ambayo ndiyo mafanikio yenyewe.
Mbili ni kufa ukiwa bado unapambania mafanikio unayotaka.
Na tatu ni kukata tamaa na kuacha kufanya.

Unajionea hapo jinsi ambavyo msamiati kushindwa haupo kabisa kwenye matokeo.
Kilichopo ni kufanikiwa au kuendelea na mapambano ya kupata mafanikio unayoyataka.

Ukienda na mpango huu wa kupambana mpaka ufanikiwe, wengi sana wataweza kupata matokeo makubwa kwenye yale wanayofanya.

Rafiki, kataa na futa kabisa msamiati kushindwa kwenye maisha yako.
Jitoe kwa kila namna kuhakikisha kwamba unafanya kwa upekee kabisa mpaka upate matokeo.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe