Habari njema Matajiri Wawekezaji,

Karibuni kwenye mfululizo wa masomo yetu ya programu ya NGUVU YA BUKU, inayotuwezesha kujenga utajiri kupitia uwekezaji kwa msimamo na muda mrefu.

Kwenye programu ya NGUVU YA BUKU ni hatua ya kuanzia kwa yeyote ambaye anataka kujifunza na kufanya uwekezaji kwa vitendo. Programu hii ina kiwango cha chini kabisa cha mtu kuwekeza ambacho ni elfu 7 kwa wiki. Hii haijalishi malengo uliyonayo kifedha.

Lengo la kiwango hiki cha chini ni asiwepo mwenye sababu ya kushindwa kuwekeza, kwa sababu tunaamini bila ya shaka yoyote kwamba kila mtu anaweza kupata elfu 1 kwa siku ya kuwekeza.

Lakini kwenye kufikia utajiri mkubwa na uhuru wa kifedha, kazi kubwa zaidi inapaswa kuwekwa. Kiasi cha mtu kuwekeza kinapaswa kuwa kikubwa na muda wa kuwekeza pia unapaswa kuwa mkubwa.

Kuwekeza kiwango cha chini cha programu na kwa muda wa miaka 10 ya kuanzia tuliyojipa ni mahali pa kuanzia. Unapokuwa na lengo kubwa zaidi, lazima uwekeze kiwango kikubwa zaidi na kwa muda mrefu zaidi.

Kwa kuona uhitaji huu mkubwa wa watu kuwajibika zaidi ili kufikia malengo makubwa ya utajiri na uhuru wa kifedha waliyonayo, tumekuja na huduma nyingine ya STAAFU NA UHURU WA KIFEDHA.

Karibu kwenye huduma maalumu ya USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI inayoitwa STAAFU NA UHURU WA KIFEDHA.

Huduma hii inawalenga wale ambao wanataka kufikia uhuru wa kifedha kwenye maisha yao ili kuishi maisha wanayoyataka, bila kulazimika kufanya kazi moja kwa moja.

Kwenye huduma hii utapewa mwongozo wa kukokotoa kiasi cha uwekezaji unachopaswa kuwa nacho kwenye umri ambao umechagua kustaafu ambacho kitakuwezesha kumudu gharama za maisha yako bila kulazimika kufanya kazi moja kwa moja.

Kisha unasaidiwa kuweka mpango wa kukuwezesha kuwa na kiasi hicho cha uwekezaji kwa kujua kiasi cha kuwekeza kila mwezi.

Utaongozwa kuweka mipango sahihi kwenye maeneo yote ya USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI ambapo ni kuongeza KIPATO, kudhibiti MATUMIZI, kuondoka kwenye MADENI na kuweka AKIBA NA KUWEKEZA.

Kwenye huduma hii utapata usimamizi wa karibu kwenye kutekeleza mipango yote ya USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI ili uweze kufikia uhuru wa kifedha kwenye muda uliopanga.

JINSI PROGRAMU INAVYOFANYA KAZI.

Programu hii ya STAAFU NA UHURU WA KIFEDHA inafanya kazi kwa mpango ufuatao;

1. Unaanza na umri ulionao sasa na umri ambao unataka uwe umefikia uhuru wa kifedha. Mfano kwa sasa una miaka 40 na unataka uwe umefikia uhuru wa kifedha ukiwa na miaka 60. Hapo una tofauti ya miaka 20.

2. Unakadiria gharama za maisha yako pale unapokuwa umefikia uhuru wa kifedha, yaani hiyo miaka 20 ijayo. Kwa kutumia kanuni maalumu inayopatikana kwenye programu hii, utajua kiasi sahihi kwa kuzingatia mfumuko wa bei kulingana na muda.

3. Ukishajua kiasi unachohitaji kuendesha gharama za maisha ukiwa umefikia uhuru wa kifedha, unakokotoa uwekezaji unaohitaji kuwa nao ili ukitoa asilimia 4 kwa mwaka itoshe kuendesha maisha yako. Asilimia 4 kwa mwaka ni kiasi cha uwekezaji wako ambacho ukitumia hutaweza kumaliza uwekezaji huo kwa kipindi chote cha maisha yako. Hivyo hata kama hufanyi kazi kabisa, bado una uhakika wa maisha mpaka unakufa, kama tu hutatumia zaidi ya asilimia 4 ya uwekezaji wako kwa mwaka.

4. Ukishajua kiasi cha uwekezaji unachopaswa kuwa nacho wakati umefikia uhuru wa kifedha, kuna kanuni maalumu ya programu hii ambayo utaitumia kukokotoa kiasi unachopaswa kuanza kuwekeza sasa ili kwa huo muda uliobaki nao uweze kufikia hicho kiwango cha uwekezaji.

5. Hapo sasa unawekwa mpango kamili ambao utaufanyia kazi, kuanzia kiasi cha kuongeza kwenye KIPATO, udhibiti wa MATUMIZI, kutoka kwenye MADENI yanayokugharimu na KUWEKEZA kila mwezi bila kuacha. Utaongozwa na kusimamiwa kwa karibu kwenye hayo maeneo yote mpaka ufikie lengo la uhuru wa kifedha.

Hii ni programu ambayo ukiifanyia kazi, matokeo yake yatakuwa ya uhakika kabisa bila ya kujali unaanzia wapi kwa sasa.

VIGEZO VYA HUDUMA

Ili kupata huduma hii ya STAAFU NA UHURU WA KIFEDHA, unapaswa kukidhi vigezo hivi vitatu, vyote kwa pamoja;

1. Una kitabu cha MTAALA WA UTAJIRI kilichoandikwa na Kocha Dr. Makirita Amani.

2. Una akaunti ya uwekezaji UTT na tayari umeshaanza kuwekeza.

3. Una uwezo na utayari wa kulipa ada ya huduma ambayo ni asilimia 10 ya kiasi unachowekeza kila mwezi (Kiasi cha chini Tsh 10,000/= na kiasi cha juu Tsh 100,000/=. Yaani kama unafanya uwekezaji mkubwa sana, ada ya juu kabisa utakayolipa ni laki moja kwa mwezi).

TOFAUTI YA NGUVU YA BUKU NA STAAFU NA UHURU WA KIFEDHA.

Swali unaloweza kuwa nalo ni ipi tofauti ya programu ya NGUVU YA BUKU na STAAFU NA UHURU WA KIFEDHA.

Kwanza kabisa ni lazima uwe kwenye programu ya NGUVU YA BUKU ndiyo uweze kupata nafasi kwenye STAAFU NA UHURU WA KIFEDHA.

Pili kwenye NGUVU YA BUKU unaenda kwa lengo la chini lililowekwa, lakini kwenye UHURU WA KIFEDHA unafanyia kazi lengo linaloendana na uhalisia wako.

Tatu kwenye NGUVU YA BUKU unasimamiwa kwenye kuwekeza tu na kutokutoa uwekezaji wako, wakati kwenye UHURU WA KIFEDHA unasimamiwa kwenye eneo zima la USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI, kuanzia kwenye KUONGEZA KIPATO, KUDHIBITI MATUMIZI, KUONDOKA KWENYE MADENI na KUTEKELEZA MKAKATI BINAFSI WA KUFIKIA UHURU WA KIFEDHA.

Nne NGUVU YA BUKU ni kwa kundi, hivyo hatua zako unashirikisha kwenye kundi, lakini kwenye UHURU WA KIFEDHA ni binafsi, hatua unazopiga unashirikisha kwa mshauri na msimamizi wako kwenye huduma.

Tano NGUVU YA BUKU ni bure, ukishakuwa na kitabu hakuna gharama ya ziada, UHURU WA KIFEDHA kuna ada ya kila mwezi kulingana na kiasi cha uwekezaji unachokuwa unafanya.

Karibu kwenye programu ya UHURU WA KIFEDHA uweze kufanyia kazi malengo ya uhakika kwako na kufikia uhuru huo.

MJADALA WA SOMO.

Karibu kwenye mjadala wa somo kushirikisha yale uliyojifunza kwa kujibu maswali haya.

1. Ipi tofauti ya programu ya NGUVU YA BUKU na UHURU WA KIFEDHA?

2. Kwa sasa una umri wa miaka mingapi?

3. Unapanga kuwa umefikia uhuru wa kifedha ukiwa na miaka mingapi?

4. Wastani wa matumizi yako kwa mwezi kwa sasa ni kiasi gani?

5. Wastani wa matumizi ya mwezi unategemea uwe kiasi gani wakati ukiwa umefikia uhuru wa kifedha?

6. Kiasi unachopaswa kuwekeza kila mwezi ili kufikia uhuru wa kifedha kwenye muda uliopanga ni ____ (hapa nitakupa jibu baada ya kukokotoa kutokana na taarifa za maswali hapo juu.)

7. Je upo tayari kwa ajili ya kuingia kwenye programu ya UHURU WA KIFEDHA? Kwa kujibu ndiyo utapewa hatua za kuingia. Kama hujawa tayari kwa sasa, shirikisha nini kinakukwamisha kwa sasa na lini utakuwa tayari.

8. Karibu kwa maswali, mapendekezo na ushauri kutoka kwenye somo hili na programu nzima ya NGUVU YA BUKU pamoja na UHURU WA KIFEDHA.

Shirikisha majibu ya maswali hayo kama uthibitisho wa kusoma somo, kulielewa na kwenda kuweka kwenye matendo.

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

+255 678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.