Habari njema muuzaji bora kuwahi kutokea,
Hongera na karibu sana kwenye mwendelezo wa makala zetu za ushawishi kutoka kwenye programu yetu ya CHUO CHA MAUZO.
Kwenye jumamosi ya ushawishi tunaongozwa na kauli mbiu yetu inayosema HUPATI UNACHOSTAHILI BALI UNACHOSHAWISHI.
Wiki iliyopita tulifanikiwa kujifunza jinsi ya kuwafanya watu wakubaliane na mawazo yako kanuni ya KUMI ambayo ni TUMIA NIA NJEMA YA WENGINE.
Na kwenye kanuni ya KUMI tulifanikiwa kuondoka na kitu kimoja ambacho ni wewe kama muuzaji bora kuwahi kutokea,
Kama unataka kuwashawishi watu wakubaliane na wewe, kama unataka watu, lenga kwenye sababu halisi kwao kufanya kitu. Na ijue nia njema kwao kufanya kile wanachofanya.
Jua nia njema ya kila mteja wako iliyoko ndani na itumie hiyo kukubaliana naye. Kuwa mdadisi wa kwa kuuliza maswali na utapata nia njema ya mtu kufanya kile anachofanya.
SOMA; Jinsi Ya Kuwafanya Watu Wakubaliane Na Mawazo Yako Kanuni Ya Kumi
Habari njema ni kwamba leo kwenye jumamosi ya ushawishi, tunakwenda kujifunza jinsi ya kuwafanya watu wakubaliane na mawazo yako kanuni ya KUMI na MOJA ambayo ni WEKA IGIZO
Mpendwa muuzaji bora kuwahi kutokea,
Mwandishi Dale Carnegie anatuambia kwamba hakuna kitu kinachotusukuma kuchukua hatua kama maigizo.
Huwa tunaangalia tamthilia na sinema na kuibua hisia kali mpaka kupelekea kucheka au kulia huku tukijua kabisa ni maigizo na siyo kweli. Maigizo yana nguvu kubwa ya kushawishi na kubadili na watu.

Hivyo basi, kama unataka uwashawishi watu wakubaliane na wewe, tumia maigizo yanayogusa hisia zao moja kwa moja.
Angalia matangazo mbalimbali ya biashara na hasa yanayowasukuma watu kuchukua hatua, huwa ni yale ambayo yanaigiza kile ambacho mtu anataka kupata. Mfano, tangazo la sabuni kwenye TV, litaonesha sabuni hiyo likitoa povu na kutakatisha nguo kuliko sababuni nyingine.
Moja kwa moja utaamini sabuni hiyo ni bora na kuinunua.
Tangazo la vilevi mbalimbali litaonesha watu wakiwa na furaha, hapo utaamini kwa kutumia kilevi hicho na wewe utakua na furaha.
Hata siku moja hutaona tangazo la kilevi likionesha picha ya mtu aliyelewa.
Kwa kile ambacho unataka mtu akubaliane na wewe na kuchukua hatua, igiza tendo ambalo litagusa hisia zake na kumsukuma kuchukua hatua.
Kwa mfano, mwandishi Dale Carnegie anatupatia mfano wa mtu aliyekuwa anauza mashine za kuhesabia fedha kwenye maduka. Alifika kwenye duka moja na kukuta wanatumia mashine ya zamani ambayo inawaingizia hasara.
Alichofanya alichukua sarafu za fedha, alizokuwa nazo na kisha kumwambia mwenye duka kwa kutumia mashine uliyonayo, umekuwa unapoteza fedha, wakati huo akirusha sarafu zile za fedha chini.
Mtu yule alimsikiliza kwa umakini na akanunua mashine mpya.
Hapa tunajifunza kitu kimoja kwamba, matendo yana nguvu kuliko maneno, na matendo hayo yanapogusa hisia, yana nguvu kali.
Mwisho, kwa kila unachotaka kuwashawishi wengine, tafuta tendo ambalo litagusa hisia zao na lifanye.
Wapo wengine ambao wamekuwa wanalia, wengine kuanguka na mengineyo ili kugusa hisia za watu wakubaliane nao.
Rafiki na mwalimu wako anayekupenda na kukujali katika mauzo,
Mwl.Deogratius Kessy
Mwalimu/Mwandishi/Mjasiriamali
Makamu Mkuu wa CHUO CHA MAUZO.
makamu@mauzo.tz, 📞0717101505//0767101504