Habari njema muuzaji bora kabisa kuwahi kutokea,

Karibu sana kwenye mwendelezo wa makala zetu za ukamilishaji ambazo ni mwendelezo wa makala kutoka kwenye programu yetu ya  CHUO CHA MAUZO.

Hongera sana kwa kuendelea kujifunza na kuchukua hatua kwa haya unayoendelea kujifunza hapa.

Leo ni jumatano ya ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu yetu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA.

Kama kauli mbiu inavyosema, mara zote unapaswa kukamilisha wateja na wewe pia unapaswa kukamilisha wateja. Na kukamilisha ndiyo wajibu wako namba moja kwenye biashara yako.
Wajibu wako namba moja ni kuuza na unapokuwa umemuuzia mteja maana yake umemkamilisha.
Hivyo basi, kila wakati wageuze wateja tarajiwa uliokuwa nao na waweze kununua na kuwa wateja kamili.

Ukamilishaji ndiyo kitu muhimu sana kwenye mauzo kwa sababu ndiyo kitu pekee kinacholeta fedha kwenye biashara kupitia kile unachouza iwe ni bidhaa au huduma.

Kwenye somo letu lililopita tulijifunza mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo nayo ni mbinu namba 45 na 46

Kwenye mbinu namba 45 tulijifunza ukamilishaji wa malipo kidogo.
Na kwenye ukamilishaji wa namba 46 tulijifunza ukamilishaji wa kuigeuza namba kuwa ndogo sana.

Na kwenye ukamilishaji wa malipo kidogo, mbinu namba 45 tulijifunza kwamba ni ukamilishaji ambao unagawa bei ya kitu kwa muda ambao atakitumia na kumwonesha mteja ni malipo kidogo anafanya. Kwa mfano, kama kitu ni cha milioni 3, ambacho atatumia kwa miaka kumi, kwa mwaka ni laki tatu na kwa mwezi ni kama elfu 25.
Kwa kuwagawa hivyo mteja anaona analipia kidogo.

Na kwenye ukamilishaji wa kuigeuza namba kuwa ndogo sana tulijifunza kwamba ni ukamilishaji wa kutumia kwenye pingamizi la bei, mara zote gawa bei kwa kiwango ambacho ni kidogo na mteja kuona anaweza kukimudu.

SOMA; Mbinu Mbili Za Uhakika Za Ukamilishaji Wa Mauzo 45-46

Leo kwenye jumatano ya ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu yetu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA, tunakwenda kujifunza mbinu nyingine mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo nazo ni mbinu namba 47 na 48.

Zifuatazo ni mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo ambazo tunakwenda kujifunza hapa;

47. Ukamilishaji wa bora kuishi tajiri.

Huu ni ukamilishaji unaomkumbusha mteja kwamba akifa ataacha kila kitu, hivyo bora kufurahia akiwa hai.

Kama mteja anakupa pingamizi lolote lile kupitia kile unachouza au huduma unayotoa labda anasema bei ni kubwa, wewe mwambie hivi;

“Ni bora kulipa zaidi na kupata unachotaka kuliko kulipa kidogo na kufanya makosa. Ni bora kuishi tajiri kuliko kufa tajiri.
Weka sahihi yako hapa na nitakuandalia bidhaa/huduma yako uanze kuifurahia mara moja, kinachofuata baada ya hapa ni wewe kukamilisha malipo, tafadhali lipia ili ukafurahie uwekezaji wako.”

48. Ukamilishaji wa hutaondoka navyo.

Ukamilishaji huu unawafanya watu kubadili mtazamo wao juu ya fedha, badala ya kuibania, wanashawishika kuitumia na kufurahia maisha yao, kwa sababu wakifa wanaziacha.

Kwa hiyo, pale mteja anapokupa pingamizi kwamba ni fedha nyingi, wewe tumia ukamilishaji huu wa hautaondoka navyo.
“Nakubaliana na wewe ni fedha nyingi, lakini jua ukifa hutaondoka na hizo fedha. Tukamilishe hili.”

Nenda leo ukawe mkamilishaji bora kabisa kuwahi kutokea na ukauze zaidi.
Shika kichwa chako na jiambie kauli hii;  Mimi … (Taja jina lako)
Ni muuzaji bora kuwahi kutokea.
Mimi ni mkamilishaji bora wa mauzo na leo ninakamilisha mauzo ya Tsh….Taja kiasi kwa kila mteja niliyemweka kwenye mchakato wa mauzo

Kutoka kwa muuzaji mwenzako, rafiki anayekupenda na kukujali,

Mwl.Deogratius Kessy

Mwalimu/Mwandishi/Mjasiriamali
Makamu Mkuu wa CHUO CHA MAUZO.
makamu@mauzo.tz, 📞0717101505//0767101504