3453; Upweke wa mafanikio.
Kutoka mezani kwa Kocha,
Rafiki yangu mpendwa,
Huwa kuna sababu za wazi zinazowazuia watu wengi kufanikiwa.
Vitu kama uvivu, uzembe na kutokujitambua vinaweza kuonekana wazi kabisa.
Lakini kuna sababu nyingine ambazo zimejificha sana, ambazo zinawazuia watu wengi kufanikiwa, japo wao wenyewe wanakuwa hawajui sababu hizo ni kikwazo kwao.
Mtu anajikuta akiweka juhudi kubwa sana, lakini bado hafanikiwi.
Ukiangalia kwa nje kila kitu kipo sawa, lakini bado mtu hafanikiwi.
Hapo ndipo unapojua kwamba ndani kuna vitu vinamzuia.
Na kama mtu hatajua vikwazo hivyo vya ndani na kuviondoa, yaani kama hataona breki zinazomzuia na akaziachilia, hataweza kupiga hatua kubwa.
Hata pale inapotokea anapiga hatua, anajikuta akijikwamisha yeye mwenyewe na kupoteza yote ambayo alikuwa ameshayajenga.
Moja ya sababu za ndani zinazowakwamisha watu kufanikiwa ni upweke wa mafanikio.
Kwa sababu mtu anakuwa amezungukwa na watu wengi ambao hawajafanikiwa, anajizuia kufanikiwa ili asiwe tofauti na wengine na akaishia kutengwa.
Kwa kuwa sisi binadamu ni viumbe wa kijamii, huwa tunajali sana kuwa ndani ya kundi la watu.
Chochote kinachoweza kuhatarisha uwepo wetu kwenye kundi la watu huwa tunakiondoa.
Ndiyo maana unapoenda mahali popote, unakuwa watu waliopo wana mfanano mkubwa kwenye mambo mengi.
Japo inakuwa haipo wazi, lakini kila mmoja anakuwa anakazana kutokutofautiana na wengine ili aendelee kukubalika kwenye kundi.
Kundi huwa lina nguvu kubwa sana ambayo mtu binafsi hawezi kuishinda.
Hasa pale kunapokuwa na ukaribu baina ya watu walio kwenye kundi, ushawishi wa wengine unakuwa mkubwa.
Unaweza kuwa na nia ya kujenga mafanikio makubwa sana kwenye maisha yako, lakini kama haupo kwenye kundi sahihi, hilo lengo lako halitaweza kufanikiwa.
KISIMA CHA MAARIFA ni jamii ya tofauti kabisa ambayo tunaijenga, yenye lengo la mafanikio makubwa kwa mtu mmoja mmoja, kundi na taifa kwa ujumla.
Unapokuwa ndani ya jamii hii, unaondoka kwenye ile hatari ya kujizuia kufanikiwa ili uendane na wengine.
Badala yake unapata msukumo wa kujenga mafanikio makubwa kutokana na hatua ambazo wengine ulionao kwenye kundi wanazipiga.
Kuwa ndani ya kundi la KISIMA CHA MAARIFA ni tiba ya mengi ambayo yamekuwa yanakukwamisha kufanikiwa.
Tumia nafasi hii vizuri ili uweze kufanya makubwa bila ya kujizuia kwa namna yoyote ile.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe