Ipo wazi kwamba, hakuna bidhaa inayokosa wateja au wateja hawapo kabisa.
Mtu yeyote anayekwambia wateja hawapo huo ni uongo wa waziwazi au ni kujifariji.
Ukweli ni kuwa, wateja wapo mara zote. Ni wewe tu kujua walipo na namna nzuri kuwafikia, kuwafuatilia na kuwauzia.

Wateja wanaweza kupungua, hilo sikatai na ni kwa sababu kuna baadhi ya vitu havijakaa sawa.
Huenda hatujulikani kwa watu sahihi, hatujaweka jitihada zaidi kuwafikia wateja wengi. Leo kwenye somo hili nimekuandalia mambo matatu kufanyia kazi;
Moja; Endelea kufanya kitu, hata kama kinakupa matokeo madogo.
Mfano, kama unapiga simu 10 unapata mteja mmoja. Ili upate wateja 2 inabidi upige simu 20. Hivyo, hapa ongeza kiwango cha kupiga simu.
Maana yake, hujaleta kitu kipya, ila umeongoza juhudi kwenye eneo lililokuwa linakupa matokeo madogo. Fanya hivyo katika maeneo mengine kama utembeleaji au utumaji wa message.
Mbili; Boresha kile kinachokupa matokeo kidogo.
Unaweza kuwa unatumia baadhi ya mbinu zinazokupa matokeo madogo muda mrefu. Ndiyo maana huoni vitu vikiwa vikubwa kama unavyotaka.
Hivyo, unachoboresha ni mbinu ulizokuwa unatumia. Mfano, “script” yako ya mazungumzo na mteja kwa maana ya uwasilishaji au ujumbe unaotuma kwa wateja.
Hii inaweza kuwa sababu ya kupata matokeo kidogo. Kwahiyo, unaandaa uwasilishaji mpya wa kutumia, lakini lengo ni lile lile.
Tatu; Fanyia kazi mbinu mpya kwenye biashara yako.
Baada ya kufanya maboresho, kama unaona bado hupati matokeo anza upya kwa namna nyingine.

Inaweza kuwa utembeleaji, kuweka status, simu, broadcast au kuingia DM kwa wateja wako. Hii pia unapima ufanisi wake.
Wakati unatumia mbinu mpya, ukiona mwanya wa kutumia ya zamani usiache. Kumbuka lengo ni kuuza.
Mbinu mpya unayotumia hakikisha ni BORA na uifanyie KAZI kwa msimamo.
Kitu kimoja zaidi, usiache kujifunza na kujifanyia tathimini juu ya matokeo unayopata na malengo yako.
Hatua za kuchukua leo; Punguza malalamiko, weka kazi kufanya kazi. Ruhusu muda uamue.
SOMA; Mtandao Unaoenda Kukupa Matokeo Makubwa Wakati Wa Ufuatiliaji
Je, ni mbinu ipi mpya ungeshauri iongezwe hapa?
Wako Wa Daima
Lackius Robert
Mkufunzi Msaidizi Chuo Cha Mauzo
0767702659 / mkufunzi@mauzo.tz