Habari njema muuzaji bora kabisa kuwahi kutokea,
Karibu sana kwenye mwendelezo wa makala zetu za ukamilishaji ambazo ni mwendelezo wa makala kutoka kwenye programu yetu ya CHUO CHA MAUZO.
Hongera sana kwa kuendelea kujifunza na kuchukua hatua kwa haya unayoendelea kujifunza hapa.
Leo ni jumatano ya ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu yetu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA.
Kama kauli mbiu inavyosema, mara zote unapaswa kukamilisha wateja na wewe pia unapaswa kukamilisha wateja. Na kukamilisha ndiyo wajibu wako namba moja kwenye biashara yako.
Wajibu wako namba moja ni kuuza na unapokuwa umemuuzia mteja maana yake umemkamilisha.
Hivyo basi, kila wakati wageuze wateja tarajiwa uliokuwa nao na waweze kununua na kuwa wateja kamili.
Ukamilishaji ndiyo kitu muhimu sana kwenye mauzo kwa sababu ndiyo kitu pekee kinacholeta fedha kwenye biashara kupitia kile unachouza iwe ni bidhaa au huduma.
Kwenye somo letu lililopita tulijifunza mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo nayo ni mbinu namba 47 na 48
Kwenye mbinu namba 47 tulijifunza ukamilishaji wa kuishi tajiri
Na kwenye ukamilishaji wa namba 48 tulijifunza ukamilishaji wa hutaondoka navyo.
Na kwenye ukamilishaji wa bora kuishi tajiri, mbinu namba 47 tulijifunza kwamba huu ni ukamilishaji unaomkumbusha mteja kwamba akifa ataacha kila kitu, hivyo bora kufurahia akiwa hai.
Na kwenye ukamilishaji wa hutaondoka navyo mbinu namba 48 tulijifunza kwamba ni ukamilishaji ambao unawafanya watu kubadili mtazamo wao juu ya fedha, badala ya kuibania, wanashawishika kuitumia na kufurahia maisha yao kwa sababu wakifa wataziacha.
SOMA; Mbinu Mbili Za Uhakika Za Ukamilishaji Wa Mauzo 47-48
Leo kwenye jumatano ya ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu yetu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA, tunakwenda kujifunza mbinu nyingine mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo nazo ni mbinu namba 49 na 50.
Zifuatazo ni mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo ambazo tunakwenda kujifunza hapa;

49. Ukamilishaji wa hakuna uhaba wa fedha.
Ukamilishaji huu unamkumbusha mteja kile kilicho muhimu zaidi. Wakati fedha zinaweza kuzalishwa kwa wingi na hakuna uhaba, kuwa na furaha ndiyo kilicho muhimu zaidi
Mteja anakupa pingamizi labda fedha nyingi, wewe unamjua hivi;
“Nakubaliana na wewe ni fedha nyingi, lakini hakuna uhaba wa fedha hapa duniani. Kuna uhaba wa watu wenye furaha na wanaopenda maisha yao. Tukamilishe hili.”
Kinachofuata baada ya ni kukamilisha malipo.
Ipi njia nzuri kwako kukamilisha malipo?
Lipia tafadhali.
50. Ukamilishaji wa sababu ya kununua.
Unatumia ukamilishaji huu pale unapokutana na mteja mgumu ambaye anaendelea kutoa mapingamizi mapya kila unapojibu mapingamizi ya awali.
Unahitaji kuwa makini kuhakikisha unamweka upande chanya na akupe sababu za kununua kisha kuzitumia kukamilisha mauzo.
“Samahani, naomba kuuliza, unatafuta sababu za kufanya maamuzi ya kununua au unatafuta sababu za kutokununua? Zipi sababu za wewe kununua?”.
Baada ya kukujibu, wewe kama muuzaji utapata majibu sahihi kama unatafuta sababu za kununua au za kutokununua.
Nenda leo ukawe mkamilishaji bora kabisa kuwahi kutokea na ukauze zaidi kupitia mbinu ulizojifunza leo na mbinu nyingine za nyuma ulizojifunza.
Shika kichwa chako na jiambie kauli hii; Mimi … (Taja jina lako)
Ni muuzaji bora kuwahi kutokea.
Mimi ni mkamilishaji bora wa mauzo na leo ninakamilisha mauzo ya Tsh….Taja kiasi kwa kila mteja niliyemweka kwenye mchakato wa mauzo
Kutoka kwa muuzaji mwenzako, rafiki anayekupenda na kukujali,
Mwl.Deogratius Kessy
Mwalimu/Mwandishi/Mjasiriamali
Makamu Mkuu wa CHUO CHA MAUZO.
makamu@mauzo.tz, 📞0717101505//0767101504