Mtaji wa kwanza unaohitaji ili kukuza mauzo yako ni wateja. Ili
uweze kuishi nao vizuri, unahitaji kujenga mahusiano mazuri.
Hii ni kwa sababu; ndio wanaonunua kwetu, wanatupa wateja wa rufaa, wanatuunganisha na wateja wengine, wanatupa kazi, vilevile wanatupa nafasi.
Ndiyo maana huwezi kuuza kama hamna wateja. Kitu kimoja zaidi, “wateja hawanunui kile unachofanya au kuuza, balihununua kwanini unafanya kitu hicho”.

Sasa ili huweze kujenga mahusiano mazuri nao kuna mambo ya kuzingatia kama nilivyoelezea hapa chini:
Moja; Unahitaji kuwa mwaminifu: Kamwe usiwe au usijaribu kuwa
muongo kwa wateja wako. Msingi mkuu wamahusiano ni uwazi na ukweli.
Umempa ahadi mteja, usikimbie. Timiza ahadi yako. Hii itamfanya pia, ajenge imani katika biashara yako. Akikuamini, ufuatiliaji wako itakupa manufaa makubwa.
Mbili; Unahitaji kuwa na subira: Mara zote sikiliza kile ambacho
mteja anaongea na usipuuze maneno yake. Huwezi kujuaubora au wazo jipya lililo ndani ya kile anachozungumza.
Usilazimishe wazo lako kupendwa au kukubaliwa namwingine ikiwa halielewi, acha usimlazimishe. Kufanyahivyo unaweza kuharibu mahusiano yako na mteja wako. Ndiyo maana tunasema, mauzo sio tukio ni mchakato. Ongea vizuri na mteja, mweleweshe vema.
Tatu; Jifunze kuhesabu maneno unayongea: Jahazi Modern Taarabu waliwahi kuimba kuwa, “Neno likishatamkwa, halirudi tena mdomoni”.
Kuwa makini na kile
unachoongea. Usimuumize mteja yeyote katika hali yoyote ile, kwa mfano, kimawazo au aina nyingine.
Mdomo unaongea lakini unaweza
kuongea maneno ya kujenga au kubomoa. Unahitajikuangalia kile unachoogea kisiharibu taswira ya biashara yako.
Nne; Kuwa na heshima:
Ukijaribu kufikiria kwa umakini
utagundua, heshima haina gharama. Haunyofoki
kucha, rangi au ngozi pale unapomheshimu mteja. Awe
mdogo au mkubwa, unapaswa kumheshimu.
Heshima kwa mteja inakujengea mahusiano makubwa, ukiwaheshimu wateja, watakuheshimu pia. Mahusianomazuri yanahitaji heshima na sio dharau.
Tano; Epuka upotoshaji:
Ikiwa unahisi mteja wako anaelekea sehemu mbaya au anaharibikiwa, usimuache akaanguka au akaharibikiwa, msaidie.
Watuwanategemea watu wengine kuwashika mkono na
kusimama nao nyakati ngumu kama vile migogoro n.k.
Usiende kutangaza kwa watu kuwa fulani amepata tatizofulani na wewe umemsaidia. Mahusiano mazuri yanahitajikutunza madhaifu ya wengine.
Sita; Kuwa na msamaha:
Wateja wana maudhi mengi, Unahitajiuwasamehe waliokukosea. Unapoweka chuki moyoni nikujibebesha mzigo mkubwa.
Weka fokasi kwenye namna gani unaweza kupata pesa yake. Vile vile unaposamehe unaufanya moyo
wako kupumua na kuruhusu kufikiria masuala mengine.
SOMA;Watu Hukunua Wewe Kabla Ya Bidhaa Yako; Jiuze Wewe Kwanza
Hatua za kuchukua leo, chagua upande chanya mbele ya mteja, ili kujenga mahusiano mazuri nao. Bila kujenga mahusiano mazuri, ufuatiliaji wako utakuwa wa shida. Maana wateja wengi hawatakupa ushirikiano.
Kumbuka wajibu wako ni kumsaidia mteja kufanya maamuzi. Huwezi kufanya maamuzi kama huna ushirikiano na wateja wako.
Wako Wako Daima
Lackius Robert
Mkufunzi Msaidizi Chuo Cha Mauzo
0767702659/ mkufunzi@mauzo.tz
Karibu tujifunze zaidi.