Kama unaweka kazi sana na bado hufanikiwi, unakosa tija.
Kazi siyo mkusanyiko tu wa juhudi, bali ni juhudi zilizoelekezwa kwa usahihi.
Anza na hamu kubwa ya matokeo unayotaka kufanya, kisha jua yale unayopaswa kufanya ili kupata matokeo hayo na fanya kwa tija kubwa.
Weka juhudi sahihi na kwa viwango vikubwa sana ili uzalishe matokeo yenye tija.
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE | +255678977007 | https://bit.ly/makirita
