Habari njema muuzaji bora kabisa kuwahi kutokea,

Karibu sana kwenye mwendelezo wa makala zetu za ukamilishaji ambazo ni mwendelezo wa makala kutoka kwenye programu yetu ya  CHUO CHA MAUZO.

Hongera sana kwa kuendelea kujifunza na kuchukua hatua kwa haya unayoendelea kujifunza hapa.

Leo ni jumatano ya ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu yetu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA.

Kama kauli mbiu inavyosema, mara zote unapaswa kukamilisha wateja na wewe pia unapaswa kukamilisha wateja. Na kukamilisha ndiyo wajibu wako namba moja kwenye biashara yako.
Wajibu wako namba moja ni kuuza na unapokuwa umemuuzia mteja maana yake umemkamilisha.
Hivyo basi, kila wakati wageuze wateja tarajiwa uliokuwa nao na waweze kununua na kuwa wateja kamili.

Ukamilishaji ndiyo kitu muhimu sana kwenye mauzo kwa sababu ndiyo kitu pekee kinacholeta fedha kwenye biashara kupitia kile unachouza iwe ni bidhaa au huduma.

Kwenye somo letu lililopita tulijifunza mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo nayo ni mbinu namba 51 na 52

Kwenye mbinu namba 51 tulijifunza ukamilishaji wa dakika za mwisho
Na kwenye ukamilishaji wa namba 52 tulijifunza ukamilishaji wa kuhalalisha.

Na kwenye ukamilishaji wa dakika za mwisho, mbinu namba 51tulijifunza kwamba ukamilishaji huu unatumika pale unapoona hakuna makubaliano yanayofikiwa. Unapaswa kuuliza mwishoni na siyo mwanzoni.

Na kwenye ukamilishaji wa  kuhalalisha mbinu namba 52 tulijifunza kwamba unatumia ukamilishaji huu kama majaribio ya kupima uwezo wa mtu kufanya maamuzi na kuhalalisha ni maamuzi sahihi kwake.

SOMA; Mbinu Mbili Za Uhakika Za Ukamilishaji Wa Mauzo 51-52

Leo kwenye jumatano ya ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu yetu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA, tunakwenda kujifunza mbinu nyingine mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo nazo ni mbinu namba 53 na 54

Zifuatazo ni mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo ambazo tunakwenda kujifunza hapa;

  1. Ukamilishaji wa kufunga.

Ukamilishaji huu unaibua mapingamizi yaliyofichwa na kuhakikisha makubaliano yaliyofikiwa hayatabadilika.

Ukamilishaji huu unamfungia mteja kwenye maamuzi aliyofanya na kumzuia asibadilike.

Kwa mfano, unamwambia mteja hivi;

“Je kuna sababu yoyote itakayokufanya ubadili mawazo yako kwenye haya maamuzi?” au “Je kuna sababu itakayokuzuia ushindwe kukamilisha leo?”

Ukamilishaji huu unakusaidia kujua mapingamizi ya mteja aliyoyafisha na kama atakuwa hana mapingamizi mengine, kitakachofuata baada ya hapo ni kumkamilisha mteja na kumwambia alipie ili aende akanufaike na huduma au bidhaa yake.

  1. Ukamilishaji wa kama niki…, je wewe uta…

Tumia ukamilishaji huu mwishoni mwa mazungumzo na siyo mwanzoni. Hii ni kumweka mteja upande chanya, kama atakubali, unakuwa umekamilisha mauzo na kinachobaki ni kujibu mapingamizi yake.

Kwa mfano, unamwambia mteja hivi;

“Kama nitaweza kujibu mapingamizi yote uliyonayo, je wewe utakuwa tayari kufanya maamuzi ya kununua?”

Kama nikikuuzia kwa bei ya washindani wangu, je utakuwa tayari kutoa oda yako sasa?

Kama nikikupunguzia bei, je utakuwa tayari kuchukua sasa?
Kama nikikupunguzia bei utakuwa tayari kulipia sasa?
Kama nikikupunguzia bei utakuwa tayari kuchukua ngapi?
Kama nikikupunguzia bei utakuwa tayari kulipia kwa miezi mingapi?

Kitu kimoja ambacho mkamilisha ji anapaswa kujua ni kwamba wateja wenye maswali na mapingamizi ndiyo wateja wazuri, maana hao wanataka kununua, ila wanachokosa ni uhakika.

Hivyo mkamilishaji anapaswa kujua kile anachouza kwa kina kiasi cha kuweza kujibu maswali na mapingamizi yote ambayo mteja anakuwa nayo.

Na katika kujibu kwake maswali na mapingamizi, anapaswa kumjengea mteja uhakika na kuamini. Ni kutokana na maswali na mapingamizi ndiyo muuzaji anaweza kujua kama mteja anahitaji ushuhuda, ofa au kingine chochote kitakachomshawishi anunue.

Rafiki, wakati sahihi wa kukamilisha mauzo kwa mteja ni pale unapoona mteja ameshapata tamaa ya kile unachomshawishi anunue.
Wajibu wako namba moja ni kuuza, NASA umakini wa mteja kugusa yale anayotaka, maumivu, maslahi ya mteja kisha ibua tamaa ya kutaka kupata kile unachomshawishi.
Bila kujua maumivu ya mteja na kuibua tamaa ya mteja ni kuibua upinzani kwa mteja kitu kitakachokuzuia kukamilisha mchakato mzima wa mauzo.

Nenda leo ukawe mkamilishaji bora kabisa kuwahi kutokea na ukauze zaidi kupitia mbinu ulizojifunza leo na mbinu nyingine za nyuma ulizojifunza.

Shika kichwa chako na jiambie kauli hii;  Mimi … (Taja jina lako)
Ni muuzaji bora kuwahi kutokea.
Mimi ni mkamilishaji bora wa mauzo na leo ninakamilisha mauzo ya Tsh….Taja kiasi kwa kila mteja niliyemweka kwenye mchakato wa mauzo

Kutoka kwa muuzaji mwenzako, rafiki anayekupenda na kukujali,

Mwl.Deogratius Kessy

Mwalimu/Mwandishi/Mjasiriamali
Makamu Mkuu wa CHUO CHA MAUZO.
makamu@mauzo.tz, 📞0717101505//0767101504