Thamani ni ubora wa kitu kutokana na hali, uhitaji na umuhimu wake.
Mfano, maji jangwani yana thamani kubwa kuliko kitu kingine chochote.
Kwenye biashara mteja anathamani kubwa kuliko kitu chochote kile, maana ndiyo hitaji la biashara. Kupitia malipo anayofanya, anasaidia biashara kukua. Na Imefunguliwa kwa ajili yake.
Ili uweze kukuza biashara na mauzo ni muhimu kuthamini maisha ya mteja katika biashara yako.
Maisha ya mteja ni muda ambao mteja anakuwa katika biashara yako. Inaweza kuwa mwaka mmoja, miwili, mitatu kutegemea na namna ya huduma unayompatia.

Tafiti zinaonyesha kwamba, wateja ni mali inayothaminiwa zaidi katika biashara yoyote ile. Hii ni kwa sababu huiwezesha biashara kupata faida.
Kumbe, kuongeza thamani ya mteja ni moja kati ya malengo muhimu ambayo biashara yako inapaswa kufanyia kazi ili kukuza mahusiano kwa wateja wako.
Ili kujua kujua na kuongeza thamani ya mteja wako unapaswa kuangalia faida ya mteja kwa mwaka zidisha wastani wa namba ya miaka atakayoendelea kuwa mteja wako.
Mfano, mteja anayekupa faida ya 100,000 kwa mwaka. Muda wa kuwa naye, tuseme miaka 5.
Utafanya hivi,
100,000×5= 500,000.
Utajikuta kwa mteja huyu kuna faida ya laki tano kwake. Ndiyo maana tunasisitiza umuhimu wa kutoa huduma nzuri kwa wateja wako na kuwa nao karibu.
SOMA; Ongeza Ufanisi Katika Huduma Kutumia Kanuni Ya 5S
Mambo muhimu kuzingatia kwenye thamani ya maisha ya mteja;
Moja; Kuwajua wateja wako.
Hii itakusaidia kuepuka kuwakwaza, kuwahudumia vibaya. Pia, itaongeza ukaribu wako kwao na kukusaidia kuweka kando wateja wasiokufaa.
Mbili; Toa huduma bora ambayo wateja hawezi kuipata katika sehemu yoyote ile.
Tatu; Tengeneza mahusiano mazuri na wateja wako, wafanye kuwa rafiki kwako na biashara yako, waone sio tu wakuja kununua, bali wanakujua kwa rafiki yako anayewajali na kuwapa kile wanachotaka.
Nne; Waelimishe wateja wako, washauri kuhusu bidhaa muhimu zinazoweza kusaidia kukuza biashara au kuboresha maisha yao.
Tano; Usipuuze faida ndogo ndogo zinapopatikana katika biashara yako.
Hitimisho;
Ni muhimu kuelewa vitu vinavyoongeza thamani ya maisha ya mteja katika biashara yako. Ili uendelee kuwa naye, kumhudumia, kumjengea imani ili baadaye akupatie wateja wengine.
Wako Wa Daima
Lackius Robert
Mkufunzi Msaidizi Chuo Cha Mauzo
0767702659/ mkufunzi@mauzo.tz.
Karibu tujifunze zaidi.