Karibu Rafiki,
Siku moja Jeff pamoja na marafiki zake watatu, walipanga kwenda kumtembelea JT ambaye waliohitimu wote chuo.

Safari yao waliianza mapema na walitegemea kufika mapema. Kwa bahati mbaya wakachelewa kutokana na sababu zilizopo nje ya uwezo wao. Giza likaingia kabla hawajafika.

Habari njema ni kuwa, Jeff alikuwa amebeba mishumaa mitano katika begi lake pamoja na kiberiti. Akawauliza wenzake kama wanachochote kinachoweza kuwasaidia mwanga. Wenzake wakasema hapana.

Baada ya kuwasikia, akawasha mshumaa ukawaka wakasogea mbele. Baada ya muda ukaisha wakati safari inaendelea.

Jeff akawasha mshumaa wa pili na watatu, safari ikaendelea. Hatimaye ukazima kabla hawajafika.

Kabla hajawasha mwingine, akawauliza tena, kweli hamna kitu kabisa kinachoweza kutusaidia kupata mwanga. Wakasema hatuna. Jeff akawaambia nipeni elfu tano tano tofauti na hapo siwashi mwingine.

Tom mmoja wao akasema, tunakupaje pesa wakati we ni mwenetu, huoni unatuonea, Ukizingatia tunakaribia kufika? Hatuna mwanga ndiyo, lakini unatapaswa kutusaidia tufike salama tuendako Jeff.

Jeff akawaambia njiti ya kiberiti imebaki moja tu. Nikiwasha ndo mwisho. Alikasirika kisa hawakumpatia pesa.

Akawasha mshumaa ukawasogeza. Ile wanakaribia kufika ukazima. Jeff hakuwasha tena mshumaa mwingine. Akawaambia njiti zimeisha. Wakasema asante hadi hapo umetusaidia.

Walitembea gizani kwa mwendo wa dakika karbia nne. Mwishowe wakafika shambani kwa kina JT rafiki yao. Huku wakifurahi na kumshukuru Jeff, japo kulikuwa na giza. Pembezoni wa shamba lile kulikuwa na shimo. Ukitembea bila mwanga unaweza kudumbukia.

Jeff ndiye alikuwa mbele yao. Ile wanashagilia wakasikia Paaa! Mtu analia. Wakaulizana kulikoni? Jeff akasema, nimedumbukia shimoni Mhh! Ngoja niwashe mshumaa. Zile kelele na mwanga wa mshumaa zilifanya JT aje haraka. Maana alikuwa nje anawasubiri.

Yaliyobakia ni historia.
Maana yangu kushirikisha hadithi hii ni kwamba, inawezekana wewe ndiye mwenye umebeba mshumaa unawaongoza watu katika biashara yako.

Huenda ni meneja, mtu wa fedha, msakaji au kitengo kingine, kuwa sehemu ya msaada wa wauzaji wenzako.

Kama biashara mna malengo yanayofanana kukuza mauzo na kutoa huduma nzuri hivyo ni muhimu;

Moja; Kuonyesha upendo kwa wauzaji wenzako.

Mbili; Kuwa sehemu ya mshauri na kiongozi wao.

Tatu; Kuwaelekeza na kuwaelewesha maeneo wasiyojua

Nne; Kuwakosoa katika njia sahihi sio kuwapoteza

Sote tunajenga nyumba moja, wateja wakipata huduma nzuri wataifurahia biashara watarudi tena. Wakirudi tena tutauza na kupata wateja wa rufaa.

Hivyo, ili kampuni na biashara ikue, tunahitaji kushikana mikono sio kuachana.

Tunahitaji kushirikiana sio kubaguana.

Mara zote tenda yale unayopenda kutendewa na wengine, usitende usiyopenda kutendewa na wengine.

Kumbuka; Huwezi kula maharage ukacheua pilau na huduma nzuri inaanzia kwenye biashara yenyewe kabla ya wateja.

Kuwa mashauri na kimbilio la Kila mmoja katika biashara yenu. Hakika mauzo yatakuwa makubwa, amani, furaha na upendo vitatawala.

Wako Wa Daima

Lackius Robert

Mkufunzi Msaidizi Chuo Cha Mauzo

0767702659 / mkufunzi@mauzo.tz

Karibu tujifunze zaidi.