Rafiki yangu mpendwa,

Ukiwa hai, hakuna siku ambayo utaacha kufikiria kuhusu fedha.

Ukiwa huna utafikiria ni jinsi gani ya kuzipata.

Na ukizipata utafikiria ni jinsi gani ya kuzitunza.

Kufikiria kuhusu fedha ni kitu ambacho tutakifanya kwa kipindi chote cha uhai wetu.

Lakini kwa bahati mbaya sana, yote tunayofikiria kuhusu fedha hayana msingi imara ambapo yamejengwa.

Badala yake ni mazoea yetu wenyewe au tuliyoiga kwa wengine.

Tumekaa darasani kwa miaka mingi, tukafundishwa mambo mengi, lakini siyo kuhusu fedha.

Tumefanya shughuli za kutuingizia fedha kwa miaka mingi, lakini hakuna kikubwa tunachoweza kuonyesha kwa upande huo wa fedha.

Yote hayo ni kwa sababu tunakosa ufunguo mkuu (master key) wa fedha na utajiri.

Tukiwa na ufunguo huo, tunaweza kufungua fursa nyingi zinazotuzunguka pale tulipo sasa na kujenga utajiri mkubwa.

Nimekuwa nakushirikisha mambo mengi sana kuhusu kujenga utajiri na uhuru wa kifedha.

Na sasa kuna fursa kubwa ya kukutana pamoja, tukajifunza kwa kina na kuweka mkakati ambao ukiufanyia kazi, utaweza kujenga utajiri kwa uhakika.

Fursa hiyo ni kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 ambayo itafanyika kuanzia tarehe 25 mpaka 27 Oktoba mwaka 2024 jijini Dar es salaam.

Hii siyo semina ya kukosa kama kweli umedhamiria kuwa na maisha ya mafanikio makubwa na yenye uhuru wa kuishi vile unavyotaka.

Ni semina ambayo utajifunza, kuweka mikakati na kusimamiwa kwa mwaka mzima katika kutekeleza mikakati yako uliyojiwekea.

Kwa maelezo zaidi kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024, tuma ujumbe kwenda namba 0717396253 sasa.

SOMA; Karibu Kwenye Semina Ya Kisima Cha Maarifa 2024; Ufunguo Wa Utajiri Na Uhuru Wa Kifedha.

Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA hapo chini nimekuelezea zaidi kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024. Karibu ujue zaidi kuhusu semina na kisha ujiwekee nafasi yako kwa kutuma ujumbe kwenda namba 0717396253.

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

+255 678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.