Rafiki yangu mpendwa,
Kwenye programu ya kujifunza na kuwekeza pamoja ya NGUVU YA BUKU, tunaamini kwamba KILA MTU ANAWEZA KUWA TAJIRI.
Hilo tuna uhakika nalo kwa sababu kwa fedha ndogo ndogo ambazo kila mtu anazipata, zikiwekezwa kwa muda mrefu kwa msimamo bila kuacha, zinaweza kujenga utajiri mkubwa.
Hiyo ni kwa sababu kinachojenga utajiri mkubwa siyo kiasi cha fedha kinachowekezwa, bali urefu wa muda ambao uwekezaji umefanywa. Pale uwekezaji unapofanyika kwa muda mrefu bila kuingiliwa, matokeo yake huwa ni makubwa sana.

Kama bado huamini, angalia hizo namba hapo chini ujionee mwenyewe.
Kwa kutumia kikokotoo cha riba mkusanyiko, shilingi elfu 1 ikitengwa kila siku na kuwekezwa, kwa riba ya asilimia 12 kwa mwaka, haya ndiyo matokeo yanayopatikana;
Mwaka 1 inakuwa Tsh 380,475.09
Miaka 5 inakuwa Tsh 2,450,090.10
Miaka 10 inakuwa Tsh 6,901,160.68
Miaka 20 inakuwa Tsh 29,677,660.96
Miaka 30 inakuwa Tsh 104,848,923.98
Miaka 40 inakuwa Tsh 352,943,175.31
Miaka 50 inakuwa Tsh 1,171,750,191.00
(NB; Ukokotoaji huu umefanyika kwa kutumia kikokotoo cha UTT AMIS kinachopatikana hapa; https://uttamis.co.tz/tools/monthly-calculator Kiasi cha kuwekezwa kila mwezi kimewekwa 30,000/= na riba ya 12% kwa mwaka ambao ndiyo wastani wa marejesho kwa mifuko ya UTT AMIS).
Unajionea mwenyewe hapo maajabu ya kuchukua hatua ndogo ndogo kwa msimamo na muda mrefu bila kuacha. Yaani elfu moja inaweza kuzaa mpaka bilioni! Kinachohitajika zaidi ni muda kuliko hata kiasi kinachowekezwa.
Unaweza kusema miaka 30 au 50 ni mingi sana. Lakini ukizingatia umri wa watu kuishi sasa, ambapo wapo wanaoishi zaidi ya miaka 80, miaka 30 mpaka 50 siyo mingi. Mtu akianza uwekezaji akiwa na miaka 30, mpaka anafika miaka 60 anakuwa amewekeza kwa miaka 30. Hivyo kuwahi kuna faida yake kubwa.
Lakini hata kwa ambao wamechelewa kuanza, bado kufanya uwekezaji kwa msimamo kuna manufaa kwao. Kwani kuwekeza kwa msimamo bila kutoa wala kuacha kwa miaka 10 na kuendelea, kuna faida kubwa sana.
SOMA; STAAFU NA UHURU WA KIFEDHA.
KARIBU KWENYE PROGRAMU YA NGUVU YA BUKU.
Programu ya NGUVU YA BUKU ni ya kujifunza na kufanya uwekezaji kwa vitendo. Lengo letu ni kufanya uwekezaji kwa kiasi kidogo kidogo (angalau elfu 1 kwa siku) na kwa muda mrefu (angalau miaka 10) kwa msimamo bila kuacha.
Kwa kuwa ndani ya programu hiyo unapata mafunzo ya uwekezaji kila wiki. Pia kila wiki unapaswa kufanya uwekezaji wa angalau Tsh elfu 7 na kutuma ushahidi kwamba umewekeza. Hilo linakupa uwajibikaji wa kuhakikisha unawekeza bila kuacha.
Habari njema ni kwamba kuwa ndani ya programu ya NGUVU YA BUKU ni bure kabisa. Huhitajiki kulipa ada yoyote kwa kipindi chote cha miaka 10 tutakayokuwa tunawekeza.
Unachohitaji ni kuwa na kitabu cha MTAALA WA UTAJIRI, ambacho kitakuwa mali yako hata kama haupo kwenye programu hii.
Kuingia kwenye programu ya NGUVU YA BUKU, wasiliana sasa na namba 0678 977 007 na utapewa maelekezo.
Chukua hatua sasa ili uweze kutumia muda kujenga utajiri mkubwa. Usikubali kuendelea kupoteza muda bila kuwekeza, njoo tuwajibishane kuwekeza kupitia programu ya NGUVU YA BUKU.
Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA hapo chini nimefafanua zaidi dhana hii ya utajiri kujengwa kwa muda na siyo kiasi kinachowekezwa. Karibu ujifunze kwa kina zaidi na uchukue hatua sahihi sasa.
Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
+255 678 977 007 / amakirita@gmail.com
MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.