3488; Kikwazo Ndiyo Kichocheo.

Kutoka mezani kwa Kocha,

Rafiki yangu mpendwa,
Vile vitu ambavyo tunaviona ni vikwazo kwetu kufanikiwa, hivyo hivyo ndiyo vichocheo vya mafanikio.

Yaani kile unachoona kinakuzuia kufanikiwa, ndiyo pia kinachoweza kukuchochea kufanikiwa.

Ndiyo maana yeyote aliyedhamiria kweli kufanikiwa hajawahi kuzuiwa na chochote.
Kwa sababu kila kinachoonekana kikwazo, ndiyo hicho hicho kinageuka kuwa njia.

Tafiti zimekuwa zinaonyesha kwamba huwa tunafanya vizuri pale tunapokuwa na uhaba wa vitu.
Pale tunapokuwa na uhuru sana, tunaishia kusumbuka na kupotea.

Pale unapokuwa na vitu kwa wingi, unashindwa kuvitumia vizuri kama ambavyo ungefanya kama vingekuwa vichache.

Unapokuwa na machaguo mengi, unashindwa kuchagua kwa usahihi.
Unapokuwa na machaguo machache, unakuwa huna namna bali kwenda na yaliyopo.

Angalia chochote kinachokukwamisha sasa na kitumie hicho kupata unachotaka.

Rasilimali ambazo una uhaba nazo, zitumie vizuri ili kupata matokeo makubwa kadiri unavyotaka.

Usilalamikie tena kwamba kuna kitu kinakuzuia, kwa sababu hicho ndiyo unapaswa kukitumia kufanikiwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe