3490; Siyo Tatizo.

Kutoka mezani kwa Kocha,

Rafiki yangu mpendwa,
Huwa kuna kauli ya Kiswahili inayosema; Ukitaka kumuua mbwa, mpe jina baya.
Kauli hiyo inatuonyesha kwamba ukikipa kitu jina, unakuwa na uhalali wa kufanya chochote unachotaka.

Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye mafanikio, kuna majina lazima uyabadilishe ndiyo uweze kufanikiwa.

Sehemu muhimu ya kubadili jina ni kwenye matatizo.
Njia bora ya kutatua tatizo lolote ni kwa kubadili jina kwanza.
Unachopaswa kufanya ni kubadili jina kutoka kuwa tatizo na kwenda kuwa changamoto.

Unapoamua kwamba tatizo siyo tatizo, unakuwa umeondoa kikwazo kikubwa sana kwenye kulitatua.

Unapoona kitu ni tatizo, unakifanya kuwa kigumu kwako kutatua.
Lakini unapoona kitu ni changamoto, kutatua inakuwa rahisi.

Chochote unachoona kinakuzuia kupata unachotaka, ni wewe mwenyewe ndiye unayekipa nguvu.

Njia ya kupunguza nguvu hiyo ni kubadili jina la kitu.
Kipe kitu jina ambalo linakifanya kionekane kuwa rahisi badala ya kuonekana kigumu.

Ni mbwa gani anayekukwamisha kwenye maisha yako ambaye unapaswa kumbadilishia jina ili uweze kumuua kihalali?
Karibu ushirikishe kwenye maoni hapo chini.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe