3494; Kubali Kuwajibishwa Ili Ufanikiwe.

Kutoka mezani kwa Kocha,

Rafiki yangu mpendwa,
Sababu mbili zinazowazuia watu kufanikiwa ni KUJUA NA KUFANYA.
Ni labda mtu hajui nini cha kufanya au anajua lakini hafanyi.

Ndiyo maana kanuni yetu kuu ya KISIMA CHA MAARIFA ni MAARIFA (kujua) + VITENDO (kufanya) = MAFANIKIO.

Tukirudi na kuangalia kwa undani zaidi tunakuta tatizo lililo kubwa zaidi ni KUFANYA.
Kutokufanya ndiyo kumewakwamisha wengi sana kwenye safari ya mafanikio.

Maana hata kama mtu anakwamishwa na kutokujua, bado jawabu lake ni kufanya.
Maana kujifunza ni kufanya.
Mtu akiwa tayari kufanya, atajifunza yote anayotaka kujua.

Kwa zama hizi za maarifa na taarifa, ambapo taarifa zinapatikana kwa urahisi sana, tayari wengi wanajua kile wanachopaswa kufanya.

Naweza kusema kwa uhakika kila mtu anajua nini anapaswa kufanya ili apate kile anachotaka.
Lakini tatizo ndiyo hilo, kutokufanya. Au mtu akianza kufanya basi kutokudumu kwenye ufanyaji.

Kama ungefanya mambo yote ambayo tayari unajua unapaswa kuyafanya, ungekuwa mbali zaidi ya hapo ulipo sasa.

Haijalishi upo chini au juu kiasi gani, kuna mengi ambayo unajua unapaswa kufanya, lakini bado huyafanyi.
Kama ungeyatekeleza yote hayo, ungekuwa umeshapata mengi unayoyataka.

Swali ni tunatokaje hapo kwenye kutokufanya?
Kwa sababu tayari tunajua, lakini kufanya ndiyo tunakwama.

Ni uwajibikaji ndiyo utakaotutoa kwenye huo mkwamo.
Peke yetu ni rahisi kujidanganya na kujifariji.
Lakini tunapowahusisha wengine, ambao hawanunui uongo wetu kirahisi, tunalazimika kufanya.

Kuwa ndani ya jamii ya KISIMA CHA MAARIFA ni njia bora ya kuwajibika kufanya.
Kuna ngazi tatu za kuwajibika ndani ya jamii hii;
Moja ni kuwajibika kwa kuahidi kwenye kundi zima kwamba utafanya kitu na kutoa ushahidi wa ufanyaji.
Mbili ni kuwajibika kwenye klabu ambapo kuna mfumo wa kufuatiliana kwa karibu.
Tatu ni kuwajibika kwa Kocha kwenye programu mbalimbali za uwajibikaji zilizopo.

MIFUMO YA UWAJIBIKAJI TULIYONAYO KWENYE KISIMA CHA MAARIFA.

1️⃣Kama unashindwa KUSOMA vitabu, ingia kwenye programu ya KURASA 10 KWA SIKU uwajibike huko.

2️⃣Kama unashindwa kufanya UWEKEZAJI, ingia kwenye programu ya NGUVU YA BUKU uwajibike huko.

3️⃣Kama unashindwa kutunza AFYA, ingia kwenye programu ya ISHI MIAKA 💯 uwajibike huko.

4️⃣Kama unashindwa kukuza KIPATO chako, ingia kwenye programu ya CHUO CHA MAUZO uwajibike huko.

5️⃣Kama unashindwa kujenga BIASHARA ISIYOKUTEGEMEA, ingia kwenye programu ya BILIONEA MAFUNZONI uwajibike huko.

6️⃣Kama unakosa watu sahihi wa kushirikiana nao kwa karibu kwenye safari yako ya mafanikio, ingia kwenye KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA uweze kuambatana na watu sahihi.

Jamii ya KISIMA CHA MAARIFA ni kifurushi kilichokamilika, kinachokugusa maeneo yote ya mafanikio.

Rafiki, ni wapi unakwama kuchukua hatua na kujizuia kufikia mafanikio makubwa unayoyataka?
Karibu ushirikishe kwenye maoni hapo chini ili tushirikishane njia bora ya kuvuka hilo.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe