3496; Pata Pesa Kwanza.
Kutoka mezani kwa Kocha,
Rafiki yangu mpendwa,
Ukitoa hewa ambayo tunapumua bure, pesa ndiyo kitu kinachofuata kwa umuhimu kwenye maisha yetu.
Na pale unapokuwa unaumwa na kuhitaji msaada kupumua, pesa ndiyo inakuwa na umuhimu wa kwanza kabisa.
Pamoja na umuhimu huo mkubwa wa pesa kwenye maisha yetu, bado watu wengi hawapo ‘siriazi’ na hili swala la pesa.
Utawasikia wakibeza pesa, wakisema maneno yasiyo mazuri kuhusu pesa.
Huku maisha yakiwa yanawaadhibu vikali sana kwa kukosa pesa.
Utawasikia watu wakisema pesa siyo kila kitu, lakini wanachelewa kulala wakitafuta pesa, wanakosa usingizi kwa sababu ya pesa na wanawahi kuamka sababu ya pesa.
Kila dakika ya maisha mtu anafikiria kuhusu pesa, halafu atakuambia pesa siyo kila kitu.
Huko ndiyo ninaita kutokuwa ‘siriazi’ na swala zima la pesa.
Maneno mengine ya kubeza harakati za kutafuta pesa kama, pesa haiwezi kununua furaha na hutaondoka nazo ukifa, nayo ni kutokuwa ‘siriazi’ na swala zima la pesa.
Na unajua pesa ikoje, iligundua huipi umakini inakukimbia.
Pesa huwa inapenda kwenda kwa wale wanaoipenda, wanaoipa umakini mkubwa.
Nitakuelewa kama utasema hayo maneno mabaya kuhusu pesa kama tayari unazo ambazo unaweza kula wewe, wajukuu wako na vitukuu bila kuimaliza kabisa.
Lakini kama ‘hutoboi’ hata mwaka mmoja wa kutumia utakavyo hata kama huingizi, basi ujumbe ni huu; KAA KIMYA NA PATA PESA KWANZA.
Weka kazi kubwa sana kwenye kuipata pesa.
Fanya zoezi la kupata pesa kuwa kipaumbele cha kwanza kwenye maisha yako.
Achana na mengine yote yanayokuondoa kwenye huo mstari wa kutafuta pesa.
Unapoanza kuwa ‘siriazi’ na pesa zako, wengi hawatakuelewa.
Utawapoteza wengi kwa sababu mtakuwa hamuendani tena.
Lakini ukishazikamata za kutosha, kila mtu atataka kuwa karibu yako.
Na hapo utaamua ufanye nini.
Lakini kwa sasa, PATA PESA KWANZA.
Rafiki, harakati za kutafuta pesa umezipa kipaumbele gani kwenye maisha yako?
Karibu ushirikishe kwenye maoni hapo chini ili tujadiliane namna ya kuzipata kwa ukubwa na uhakika.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe