Teknolojia Mpya Unayoweza Kuigeuza Kuwa Msaidizi Wako Binafsi (Personal Assistant).

Rafiki,
Maisha yetu hapa duniani yamekuwa yanarahisishwa sana na mapinduzi ya teknolojia.

Binadamu tulianza kwa kula matunda na mizizi.
Baadaye ikaja teknolojia ya mawe, ambayo yalitumika kama zana za kazi.

Tukaenda na mawe ambayo kufanyia kazi ilikuwa vigumu. Mpaka pale ilipogunduliwa chuma na kurahisisha zaidi utendaji kazi.

Watu walitumia chuma kupata zana bora zaidi, lakini bado walilazimika kutumia nguvu za mwili kwenye zana hizo.
Ni mpaka ugunduzi wa viwanda ulipokuja ndiyo uzalishaji uliweza kuwa mkubwa sana.

Mapinduzi ya viwanda yalionekana kama ndiyo mwisho wa teknolojia, lakini ujio wa kompyuta na mtandao wa intaneti ulivuruga hilo kabisa. Kwani ilirahisisha sana kazi na kuongeza uzalishaji.

Rafiki, kwenye mapinduzi yote hayo ya nyuma, wale waliokuwa wanayawahi ndiyo walikuwa wananufaika.

Tumekuwa kwenye mapinduzu ya kompyuta na intaneti kwa muda sasa, na hatimaye mapinduzi mapya yanatokea.
Haya ni mapinduzi ya eneo la akili, ambapo sasa tunaweza kutengeneza akili zinazoweza kurahisisha sana mambo yetu.

Hiyo inaitwa Akili Mnemba (Artificial Intelligence) ambayo kwa sasa inaleta mapinduzi makubwa sana.

Akili mnemba inaweza kufundishwa na kutekeleza majukumu mengi ambayo yanafanywa na watu sasa.

Inaweza kuandika, kuchora, kuimba, kushauri, kutibu, kufundisha na hata kuburudisha.

Hii video imetengenezwa kwa akili mnemba, kwenye darasa utajifunza jinsi ya kufanya hivyo.

Kama ilivyokuwa kwa mapinduzi ya nyuma, wale waliokuwa wanayawahi ndiyo waliokuwa wananufaika.

Na hapo ndipo penye fursa nzuri kabisa kwetu, kwani kwenye Akili Mnemba ndiyo kwanza mapinduzi yenyewe yanaanza.

Tupo hatua za awali kabisa za haya mapinduzi. Ambapo tukielewa na kuchukua hatua haraka, basi tutapata manufaa makubwa.

Ni kwa kugundua umuhimu wa mapinduzi haya, tumekuandalia darasa la IJUE AKILI MNEMBA litakalofanyika kupitia kundi la KISIMA CHA MAARIFA.

Darasa hilo linakwenda kukupa uelewa wa Akili Mnemba na jinsi ya kuitumia kukusaidia majukumu ambayo kwa sasa unawalipa watu wayafanye.

Kwa kushiriki darasa hili utaweza kuipa maelekezo akili mnemba na kutekeleza majukumu yako mbalimbali.

Picha hii imetengenezwa kwa kutumia akili mnemba. Kwenye darasa utajifunza jinsi ya kufanya hivyo.

Darasa hilo litakuwa siku ya jumamosi, tarehe 03/08/2024 kuanzia saa moja kamili jioni.
Darasa linafanyika kwa njia ya mtandao, kupitia kundi la Whatsapp la KISIMA CHA MAARIFA.

Kushiriki darasa hilo ni bure kabisa kwa wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA.
Kama tayari ni mwanachama jiandae na darasa.

Kama bado hujawa mwanachama, jiunge sasa bure kwa kutumia kiungo hiki; https://chat.whatsapp.com/KHtzXfz8pR85ZTHtJ8ZmS4

Rafiki, mapinduzi ya nyuma hukuwepo, hivyo hukunufaika nayo.
Usikubali haya mapinduzi yanayoendelea sasa hivi yakupite.

Ungana nasi jumamosi tarehe 03/08/2024 saa moja jioni hapa; https://chat.whatsapp.com/KHtzXfz8pR85ZTHtJ8ZmS4

Darasa hili limeandaliwa na Latyankiira Shoo kwa kushirikiana na Kocha Dr. Makirita Amani.

Usipange kukosa fursa hii ya kipekee kwako kujua na kutumia Akili Mnemba kutengeneza msaidizi wako binafsi.