Habari njema wauzaji kuwahi kutokea.
Karibu katika mwendelezo wa masomo yetu hapa Chuo Cha Mauzo, yenye kutufanya kuwa wauzaji bora kuwahi kutokea na kukuza mauzo yetu.
Leo tutajifunza ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia matukio ya kitaifa kama sababu ya kuwasiliana na wateja wetu.

Matukio ya kitaifa, ni mfulululizo wa matukio mbalimbali yanayofanyika nchini kulingana na kalenda husika. Matukio haya yanaweza kuwa sherehe, kumbukizi za mambo yaliyofanyika na husherekewa kitaifa na wananchi wote.
Mfano wa matukio ya kitaifa ni kama Nane Nane, Saba Saba, uhuru muungano na matukio mengine mengi.
Uzuri wa matukio haya kila mmoja anakuwa anayafahamu. Hivyo, unapofanya mawasiliano nao katika siku husika unawafanya wajisikie vizuri.
Jinsi ya kutumia matukio ya kitaifa kuwafuatilia wateja wako;
Moja; Unapitia kwenye status, mitandao yao ya kijamii na kutoa maoni.
Mbili; Andaa ujumbe wa salamu utaowatumia wateja wako
Tatu; Andaa mpango mkakati wa kuwasiliana na wateja wako. Hapa jua muda mzuri kupiga au kuwasiliana na wateja wako.
Faida za kutumia matukio ya kijamii kuwafuatilia wateja wako.
Moja; Mapokeo mazuri.
Hii inajitokeza baada ya mwendelezo wa mawasiliano ya mara kwa mara kwa wateja wako.
Mbili; Umakini.
Siku ina saa 24 zenye mambo mengi tofauti yanayojitokeza. Ndani ya siku yake anapona ujumbe wako kumpongeza kuna namna anaongeza umakini kwako.
Tatu; Ushirikiano.
Binadamu mara nyingi tunapenda watu wanaotuonyesha ushirikiano mkubwa kwetu, hata sehemu ya matukio haya ni rahisi kukupa ushirikiano katika masuala mengine
Nne; Kumbukizi nzuri.
Kila mtu kwenye siku yake yapo mambo mengi ya kufanya. Mtu anapoandaa ujumbe au kuwasiliana na wewe ina maana anakukumbuka.
Kama anakukumbuka basi anakuthamini, akikuthamini na biashara yako ataithamini.
SOMA; Tumia mitando ya kijamii kuwafuatilia wateja
Hatua za kuchukua leo; Andaa orodha ya wateja wako unaotaka kuwasiliana nao, kuwapigia simu au kuwatembelea pia, andaa ratiba yako kulingana na matukio yanayoendelea, ili iwe rahisi kuyakumbuka na kuyatumia kama sababu ya kuwafikia wateja wako.
Wako Wa Daima
Lackius Robert
Mkufunzi Msaidizi Chuo Cha Mauzo.
0767702659/ mkufunzi@mauzo.tz
Karibu tujifunze zaidi.