3515; Akili na Jitihada.

Kutoka mezani kwa Kocha,

Rafiki yangu mpendwa,

Watu huwa wanasema ili kufanikiwa unapaswa kufanya kazi kwa akili (work smart) na siyo kufanya kazi kwa juhudi kubwa (work hard).

Hivyo huwa ni vitu rahisi kusema kwa nadharia, lakini inapokuja kwenye uhalisia mambo huwa ni tofauti kabisa.

Kwenye uhalisia inadhihirika kwamba pamoja na kutumia akili nyingi, bado jitihada kubwa zinahitajika kwenye kukamilisha majukumu mbalimbali.

Mafanikio ya mtu yanategemea sana;
1. Msukumo wa ndani anaokuwa nao mtu kwenye kupiga hatua kubwa. Hili huwa haliwezi kuigwa wala kufundishwa.
2. Kuwa na nguvu ya kuweza kuweka juhudi ili kupata kile ambacho mtu anakitaka.
3. Mtazamo chanya juu ya mtu mwenyewe, kile anachofanya na maisha kwa ujumla.
4. Maamuzi sahihi kwenye mambo mbalimbali, hayo yanasaidia kuamua vyema kwenye mambo mengi.
5. Imani kali juu ya kile ambacho mtu anataka kupata au kufikia, kuamini kwamba inawezekana.
6. Mapenzi ya dhati kwenye kile ambacho mtu anafanya, ambayo yanapelekea mtu awe na shauku kwenye ufanyaji.

Unaona hapo jinsi ambavyo akili ni sehemu ndogo tu ya mafanikio. Sehemu kubwa imebebwa na jitihada ambazo mtu anapaswa kuziweka.

Badala ya kujidanganya kwamba unafanya kazi kwa akili na siyo nguvu, kubali kufanya kazi kwa akili nyingi na jitihada kubwa sana.
Yote mawili yanahitajika kwa pamoja na muingiliano mkubwa ili mtu aweze kupata mafanikio makubwa.

Rafiki, umekuwa unatumiaje akili na jitihada kwa pamoja ili kujijengea mafanikio makubwa unayotaka kufikia?
Karibu ushirikishe kwenye maoni hapo chini ili uweze kutumia yote kwa pamoja kwa manufaa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe