Rafiki yangu mpendwa,

Njia bora kabisa ya kujifunza kwenye maisha ni kutoka kwa wale waliofanikiwa kwenye kitu hicho.

Inapokuja kwenye uwekezaji, Warren Buffet, bilionea na mwekezaji ambaye amekuwa na mafanikio makubwa kwa zaidi ya miaka 70 akiwa mwekezaji, ni mtu sahihi wa kumsikiliza.

Ushauri ambao Buffett amekuwa anatoa kwenye uwekezaji umebebwa na kauli yake hii;

    “Uwekezaji bora kabisa unauweza kufanya, ni kuwekeza ndani yako mwenyewe. Huo ndiyo uwekezaji utakaodumu na kukupa faida kubwa.”

Kinachofanya uwekezaji ndani yako uwe bora ni;

1. Hakuna anayeweza kukunyang’anya, ulichojifunza kitabaki na wewe milele.

2. Hutatozwa kodi kwenye uwekezaji huo, ukishajua umejua.

3. Thamani yake haiathiriwi na mfumuko wa bei, bali unazidi kuwa mbele ya mfumuko.

Wekeza kwako mwenyewe kwa kujifunza na kujijengea ujuzi ambao utakufanya kuwa bora zaidi.

Kwenye kuwekeza ndani yako mwenyewe, mwaka huu 2024 kuna fursa bora kabisa ambayo hupaswi kuikosa.

Fursa hiyo ni SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024.

Semina hii inakwenda kukupa maarifa sahihi ya KUPATA, KUTUNZA na KUZALISHA fedha kwa kutumia nguzo saba unazopaswa kuzijua.

Nguzo hizo saba za kukuwezesha kuwa imara kifedha ni kama ifatavyo;

1. KIPATO; Kikubwa, Uhakika na Endelevu.

2. AKIBA; Dharura, Malengo na Nidhamu.

3. MATUMIZI; Mahitaji, Matakwa na Anasa.

4. MADENI; Mazuri, Mabaya na Kutokomeza.

5. MATOLEO; Sadaka, Misaada na Kodi.

6. UWEKEZAJI; Masoko, Hatifungani na Mali.

7. ULINZI (BIMA); Afya, Mali na Maisha

Kwenye nguzo hizo saba unakwenda kujifunza kwa vitendo na kutoka na hatua za kwenda kuchukua ili uwe imara kifedha.

Hupaswi kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 kama upo makini na fedha zako.

Semina itafanyika Mbezi Garden Hotel DSM tarehe 27/10/2024.

Ada ya kushiriki semina ni Tsh 65,000/= Kama utalipa kabla ya tarehe 01/10/2024 na kuanzia tarehe 01/10/2024 ada ya kushiriki itakuwa Tsh 100,000/=.

Kushiriki piga simu au tuma ujumbe wa kawaida au kwa wasap kwenda namba 0752977170 wenye maneno SEMINA 2024 na utapewa utaratibu mzima na nafasi ya kushiriki.

Karibu rafiki uchukue hatua sasa ili kufanya uwekezaji bora kabisa kwako, utakaoacha alama kubwa kifedha kwako.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi