Rafiki yangu mpendwa,
Najua changamoto zako zote za kifedha umekuwa unalaumu kipato ambacho unaingiza.
Kama kipato hakitoshelezi matumizi, unaona kwamba kipato kingekuwa kikubwa basi ungeweza kutosheleza matumizi. Lakini umekuwa unaongeza kipato kila mara na matokeo yake ni matumizi nayo kuongezeka.
Kama umekuwa huweki akiba, unaona ni kipato kidogo hivyo huna cha kuweka akiba. Lakini pia kipato kimekuwa kinaongezeka na hujawahi kubakisha akiba.
Na kama huwekezi, unaweza kuona ni kwa sababu huna unachoweza kuwekeza kwenye kipato chako. Lakini kipato hicho hicho kuna makato umekuwa unakatwa kwa lazima na bado maisha yanakwenda.

Rafiki, mambo mengi unayokwama kifedha, tatizo siyo fedha au kipato unachoingiza, bali tatizo ni wewe mwenyewe. Kwa namna ulivyo na unavyochukulia kipato, imekuwa inakukwamisha.
Leo nina habari njema sana kwako za jinsi ya kutatua changamoto zako binafsi ulizonazo kifedha ili uweze kuongeza kipato chako, kuweka akiba kwenye kila kipato na kufanya uwekezaji.
Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 unakwenda kupata nafasi ya kujifunza hayo kwa kina na vitendo ili ubadili maisha yako.
Karibu sana ushiriki semina hii na uweze kuleta mabadiliko ya kweli kwenye maisha yako.
Karibu Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024.
Semina hii inakwenda kukupa maarifa sahihi ya KUPATA, KUTUNZA na KUZALISHA fedha kwa kutumia nguzo saba unazopaswa kuzijua.
Nguzo hizo saba za kukuwezesha kuwa imara kifedha ni kama ifuatavyo;
1. KIPATO; Kikubwa, Uhakika na Endelevu.
2. AKIBA; Dharura, Malengo na Nidhamu.
3. MATUMIZI; Mahitaji, Matakwa na Anasa.
4. MADENI; Mazuri, Mabaya na Kutokomeza.
5. MATOLEO; Sadaka, Misaada na Kodi.
6. UWEKEZAJI; Masoko, Hatifungani na Mali.
7. ULINZI (BIMA); Afya, Mali na Maisha
Kwenye nguzo hizo saba unakwenda kujifunza kwa vitendo na kutoka na hatua za kwenda kuchukua ili uwe imara kifedha.
Hupaswi kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 kama upo makini na fedha zako.
Semina itafanyika Mbezi Garden Hotel DSM tarehe 27/10/2024.
Ada ya kushiriki semina ni Tsh 65,000/= Kama utalipa kabla ya tarehe 01/10/2024 na kuanzia tarehe 01/10/2024 ada ya kushiriki itakuwa Tsh 100,000/=.
Kushiriki piga simu au tuma ujumbe wa kawaida au kwa wasap kwenda namba 0752977175 wenye maneno SEMINA 2024 na utapewa utaratibu mzima na nafasi ya kushiriki.
Karibu rafiki uchukue hatua sasa ili kufanya uwekezaji bora kabisa kwako, utakaoacha alama kubwa kifedha kwako.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
