3549; Ushindi ni kutokuacha.

Kutoka mezani kwa Kocha,

Rafiki yangu mpendwa,

Watu wawili, wanaweza kuanza kitu kimoja, wakianzia kwenye ngazi inayofanana.
Lakini baada ya muda mrefu, unakuta mmoja amefanikiwa kwenye kitu hicho, wakati mwingine hayupo kabisa.

Unapowaangalia watu hao, huoni chochote ambacho ni tofauti kubwa baina yao.
Lakini matokeo wanayokuwa wameyapata ni tofauti kabisa.

Kitu kikubwa kinachowatofautisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa ni mwendelezo wa kufanya kile walichochagua.

Sehemu kubwa ya mafanikio kufanya kwa mwendelezo bila kuacha.
Pale mtu anapochagua kufanya kitu na kuendelea kufanya bila ya kuishia njiani, anajiweka kwenye nafasi kubwa ya kufanikiwa kwenye kitu hicho.

Ni kufanya kwa muda mrefu bila kuacha ndiyo kunakuweka kwenye nafasi nzuri ya kupata mafanikio makubwa.

Kama kuna somo moja unaloweza kupata kuhusu mafanikio na likawa na tija kwako ni usiache kufanya.

Ukipata matokeo mazuri, endelea kufanya.
Na hata ukipata matokeo mabaya, endelea kufanya.

Endelea kufanya kwa msimamo bila kuacha na utakuwa umejiweka kwenye nafasi nzuri ya kupata mafanikio unayoyataka.

Rafiki, ni nini ambacho umechagua kukifanya kwa msimamo bila kuacha hata iweje? Hicho ndicho chenye mafanikio makubwa unayoyataka, komaa nacho.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE
+255 678 977 007 | http://www.amkamtanzania.com

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe