Rafiki yangu mpendwa,

Kuna vipindi unaweza kuwa huna fedha, maisha yanakuwa magumu, lakini kuna matatizo ya aina fulani ambayo hayakusumbui kwenye vipindi hivyo.

Unakuwa na mipango mizuri sana ambayo utaitekeleza unapopata fedha. Lakini cha kukushangaza ni jinsi ambavyo ukipata fedha, matatizo yanaanza kujitokeza.

Unakuja kushtuka fedha zimeishia kwenye kutatua matatizo na mipango yote uliyokuwa nayo haijaweza kutatuliwa. Hili limekuwa linajirudia rudia, kila unapopata fedha, matatizo nayo yanaibuka na kutumia fedha zote.

Rafiki, kama umechoshwa na hilo lakini hujaweza kulitatua, nina habari njema kwako. Lakini kabla sijakupa hizo habari njema nikuambie kwa ufupi sana kwa nini ukipata fedha na matatizo yanakuja.

Ukiwa huna fedha, matatizo huwa yanakuwepo, lakini kwa sababu huna namna ya kuyatatua, mengi unayapuuza. Ukiwa na fedha, matatizo yale yale yanakuwepo, lakini kwa kuwa una njia ya kuyatatua, unatumia fedha ulizonazo kuyatatua.

Hivyo tatizo siyo fedha kuleta matatizo, bali ni mtazamo wako kwenye matumizi ya fedha kutatua matatizo. Na hilo tatizo la kimtazamo ulilonalo ndiyo tunakwenda kulitatua siku ya tarehe 27/10/2024.

Hiyo ni siku ambayo hupaswi kuikosa kama umechoshwa na hali ya kifedha uliyonayo sasa na ungependa kuibadili.

Karibu Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024.

Semina hii inakwenda kukupa maarifa sahihi ya KUPATA, KUTUNZA na KUZALISHA fedha kwa kutumia nguzo saba unazopaswa kuzijua.

Nguzo hizo saba za kukuwezesha kuwa imara kifedha ni kama ifuatavyo;

1. KIPATO; Kikubwa, Uhakika na Endelevu.

2. AKIBA; Dharura, Malengo na Nidhamu.

3. MATUMIZI; Mahitaji, Matakwa na Anasa.

4. MADENI; Mazuri, Mabaya na Kutokomeza.

5. MATOLEO; Sadaka, Misaada na Kodi.

6. UWEKEZAJI; Masoko, Hatifungani na Mali.

7. ULINZI (BIMA); Afya, Mali na Maisha

Kwenye nguzo hizo saba unakwenda kujifunza kwa vitendo na kutoka na hatua za kwenda kuchukua ili uwe imara kifedha.

Hupaswi kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 kama upo makini na fedha zako.

Semina itafanyika Mbezi Garden Hotel DSM tarehe 27/10/2024.

Ada ya kushiriki semina ni Tsh 65,000/= Kama utalipa kabla ya tarehe 01/10/2024 na kuanzia tarehe 01/10/2024 ada ya kushiriki itakuwa Tsh 100,000/=.

Kushiriki piga simu au tuma ujumbe wa kawaida au kwa wasap kwenda namba 0752977175 wenye maneno SEMINA 2024 na utapewa utaratibu mzima na nafasi ya kushiriki.

Karibu rafiki uchukue hatua sasa ili kufanya uwekezaji bora kabisa kwako, utakaoacha alama kubwa kifedha kwako.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi