3559; Watu, Michakato na Zana.
Kutoka mezani kwa Kocha,
Rafiki yangu mpendwa,
Mafanikio ni pishi ambalo linahitaji viungo muhimu kwa mchanganyiko sahihi.
Watu wengi wamekuwa hawaelewi hili na hivyo kujikuta wakihangaika na mengi yasiyokuwa na tija.
Mafanikio makubwa kwenye maisha huwa ni matokeo ya kuwapanga vizuri watu, kuboresha michakato na kutumia zana kama nyenzo sahihi.
Vitu hivyo vitatu ndivyo vinavyounda mfumo mzima wa mafanikio.
WATU
Unahitaji watu sahihi na uwaweke kwenye maeneo sahihi ili waweze kukupa matokeo unayoyataka.
Ukubwa wa mafanikio yako unategemea sana ubora wa watu unaoshirikiana nao.
Kama huwezi kuchagua watu sahihi na kuwapanga vizuri, utakwama kwenye mengi.
MICHAKATO.
Kwenye kila unalofanya, kuna michakato ambayo umekuwa unaitumia kwenye ufanyaji.
Michakato hiyo imekuwa inakupa matokeo, lakini je hayo ndiyo matokeo bora zaidi unayoweza kuyapata?
Unapaswa kuwa unaboresha kila mchakato unaoufanyia kazi.
Watu wengi huwa wanapenda kufanya mambo kwa mazoea, kitu kinachowapa matokeo madogo.
Kila wakati unapaswa kuwa unaboresha michakato yako ili ikupe matokeo bora zaidi.
ZANA.
Mafanikio makubwa yanahitaji nyenzo, ambapo juhudi kidogo unazoweka zinazalisha matokeo makubwa.
Hilo linawezekana kama mtu utakuwa na zana sahihi unazotumia kwenye yale unayofanya.
Zana zinapaswa kuwa bora ili kuzalisha matokeo makubwa.
Kwa maendeleo makubwa ya teknolojia yaliyopo, kuna zana nyingi bora za kukuwezesha kupata matokeo makubwa.
Wajibu wako ni kila wakati kuhakikisha zana unazotumia ndiyo bora zaidi kwenye kile unachofanya.
Rafiki, unatumiaje WATU, MICHAKATO na ZANA kuzalisha matokeo makubwa na ya tofauti?
Ni kwa kuleta pamoja vitu hivyo vitatu ndiyo unaweza kupata mafanikio makubwa kwenye chochote unachofanya.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE
+255 678 977 007 | http://www.amkamtanzania.com
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe